Mgonjwa anakhofia madhara akioga baada ya kuota ndoto ya jimaa

Swali: Siku mbili baada ya kufanyiwa upasuaji niliota ndoto ya kujamii na nikakhofia kwamba nikoga huenda nikapata madhara, bila kumuuliza daktari kama kuoga kungeleta madhara au hapana. Lakini nilichukua mawe kutoka katika ua wa hospitali na kuyaweka kwenye mfuko, kisha nilitawadha kwa kuwa nilikuwa na uwezo wa kufanya hivyo, halafu nikafanya Tayammum badala ya kuoga. Niliendelea na hali hiyo kwa siku mbili, kisha nikaoga, lakini niliendelea kutawadha na kufanya Tayammum kwa pamoja, kwa kuwa maji hayakufika kwenye mwili wangu wote. Je, nilichofanya ni sahihi au inanilazimu kurudia?

Jibu: Kuacha kuosha mwili wako wote baada ya kuota ndoto ya kutokwa na manii haijuzu. Bali ilikupasa kuoga na uepuke kutumia maji kwenye sehemu ya upasuaji ambayo ulikhofia kupata madhara. Kwa hiyo ni lazima kurudia swalah ulizoswali kabla ya kuoga. Katika hali kama hiyo, unatakiwa kufanya Tayammum kwa ajili ya sehemu ya upasuaji ambayo maji hayakuifikia.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/302)
  • Imechapishwa: 23/11/2026