Sentesi moja upande wa kulia, sentesi nyingine upande wa kushoto

Swali: Je, muadhini ageuke upande wa kulia na upande wa kushoto wakati anaposema:

حَيَّ عَلى الصلاةِ

“Njooni katika swalah.”

kisha tena ageuke upande wa kulia na wa kushoto wakati ataposema tena:

حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ

“Njooni katika mafanikio.”

au ageuke kuliani wakati wa kusema:

حَيَّ عَلى الصلاةِ

“Njooni katika swalah.”

na ageuke kushoto wakati wa kusema:

حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ

“Njooni katika swalah.”?

Jibu: Baadhi wanasema kuwa atageuka kuliani peke yake wakati wa kusema:

حَيَّ عَلى الصلاةِ

“Njooni katika swalah.”

na kushotoni peke yake wakati wa kusema:

حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ

“Njooni katika swalah.”

Wengine wakasema kuwa atageuka kuliani wakati wa kusema:

حَيَّ عَلى الصلاةِ

“Njooni katika swalah.”

pale mara ya kwanza, na kushotoni pale ataposema hivo kwa mara ya pili. Halafu wakati wa kusema:

حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ

“Njooni katika swalah.”

atageuka kuliani pale mara ya kwanza, na kushotoni pale mara ya pili ili kila upande aupe sehemu ya ujumbe wake. Hata hivyo kilichotangaa na kinachoafikiana na Sunnah ni kwamba wakati wa:

حَيَّ عَلى الصلاةِ

“Njooni katika swalah.”

atageuka upande wa kulia peke yake katika zile mara mbili zote, na kwamba wakati wa:

حَيَّ عَلى الْفَلاَحِ

“Njooni katika swalah.”

atageuka upande wa kushoto peke yake katika zile mara zote mbili. Yale yanayofanywa na baadhi ya waadhini wanasema sentesi hizo kisha ndio wanageuka hayana msingi wowote.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/175)
  • Imechapishwa: 09/04/2026