Swali: Vipi kuhusu kuwachukua wanawake na watoto pia kumtolea salamu Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kwa nyuma?

Jibu: Wanaume ni Sunnah kumtolea salamu (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) mbele ya uso wake, kisha ageuke kidogo kwa Abu Bakr as-Swiddiyq, kisha ageuke kidogo kwa ´Umar  bin al-Khattwaab (Radhiya Allaahu ´anhumaa). Hiyo ndio Sunnah. Kuhusu wanawake hapana haitakiwi wao kutoa salamu. Watoto wanaojua kusalimia wasalimie pamoja na wanaume. Kuhusu wanawake Sunnah ni wao kutotoa salamu. Serikali inawachukulia wepesi, kwa sababu baadhi ya maimamu wanawajuzishia wanawake kuyatembelea makaburi. Kwa ajili hiyo serikali inawachukulia wepesi juu ya mada hii. Hata hivyo maoni yenye nguvu ni kwamba wanawake hawatakiwi kulitembelea, ni mamoja kaburi lake wala la kaburi la mwengine. Kumepokelewa Hadiyth ya kwamba Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amewalaani wanawake wenye kuyatembelea makaburi. Hadiyth hiyo ni yenye kuenea. kuhusu maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):

”Yatembeleeni makaburi, kwani yanakukumbusheni Aakhirah.”

ni maalum kwa wanaume. Wanaume ndio wanaozungumzishwa. Haya ndio maoni yenye nguvu.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24591/حكم-سلام-النساء-والاطفال-على-النبي-ﷺ
  • Imechapishwa: 12/11/2024