Salamu kwa kuashiria mkono

Swali: Ni ipi hukumu ya kutoa salamu kwa kuashiria na mkono?

Jibu: Haijuzu kutoa salamu kwa kuashiria. Sunnah ni kutoa salamu kwa maneno kwa mkono na katika kuitikia. Kuhusu kutoa salamu kwa kuashiria ni jambo lisilofaa. Kwa sababu ni jambo linalofanana na vitendo vya baadhi ya makafiri. Isitoshe ni kwenda kinyume na yale aliyoweka Allaah katika Shari´ah. Lakini ni sawa endapo atatamka na kumwashiria muislamu aliyeko mbali kwa mkono wake ili aweze kufahamu kuwa anamsalimia pamoja. Kwa sababu kumepokelewa yanayofahamisha juu ya hilo. Vivyo hivyo pale ambapo muislamu atakuwa ameshughulishwa na swalah basi atajibu kwa kuashiria. Hivyo ndivo ilivyosihi Sunnah kutoka kwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam).

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (06/444)
  • Imechapishwa: 25/02/2021