11- Shurayh al-Kindiy amesema:

Nimewaona waume wenye kuwapiga wake zao

mkono wangu upooze nikimpiga Zaynab

Zaynab ni jua na wanawake wengine wote ni nyota

pindi jua linapochomoza nyota zinapotea[1]

12- Kulisemwa kuambiwa Muhammad bin al-Hanafiyyah:

“Ni kwa nini unakasirika?” Akajibu: “Ili nionekane kijana kwa ajili ya wanawake.”[2]

13- ad-Daaraqutwniy amesema:

“Imesemekana kuwa Sulaym bin ´Itm alikuwa akisoma Qur-aan nzima mara tatu kila usiku  na akimjamii mke wake na kuoga mara tatu. Alipofariki mwanamke wake alisema: “Allaah akurehemu! Hakika ulikuwa ukimridhisha Mola wako na ukimridhisha mke wako.”[3]

14- Ibn Abiyz-Zinaad ameeleza kutoka kwa baba yake ambaye amesema:

“Watoto wa az-Zubayr ´Abdullaah, Musw´ab na ´Urwah walikusanyika ndani ya Hijr ya Ibn ´Umar. Ibn ´Umar akasema: “Tamanini.” ´Abdullaah akasema: “Natamani ukhaliyfah.” ´Urwah akasema: “Natamani elimu ichukuliwe kutoka kwangu.” Musw´ab akasema: “Natamani kuchukua mamlaka ya ´Iraaq na kukusanya kumuoa ´Aaishah bint Twalhah na Sukaynah bint al-Husayn.” Ibn ´Umar akasema: “Kuhusu mimi natamani msamaha.” Kila mmoja akapata kile alichotamani na pengine Ibn ´Umar amesamehewa.”[4]

15- Imesemekana kwamba ´Umar bin ´Ubaydillaah alimnunua mjakazi kwa 100.000. Wakati alipoona kuwa mwanamke huyo amesikitika kwa sababu ya kutengana na mmiliki wake akamwambia mmiliki huyo:

“Mchukue na baki na pesa.”

16- Bishr bin Kathiyr amesema:

“Mke wa Mutwarrif bin ´Abdillaah amenihadithia kwamba alimuoa kwa 30.000, nyumbu, kitambara na mtengeneza nywele.”[5]

Ghaylaan amesema:

“Mutwarrif alimuoa mwanamke kwa 20.000.”

17- Yasaar bin ´Abdir-Rahmaan amesema:

“Sa´iyd bin al-Musayyab alimuoza msichana wake kwa mvulana wa kaka yake kwa dirhamu mbili.”[6]

18-  ´Aliy bin Zayd amesema:

“Sa´iyd bin al-Musayyab amesema: “Shaytwaan hakati tamaa juu ya kitu isipokuwa hukiendea kupitia kwa wanawake.” Kisha Sa´iyd akasema: “Hakuna kitu ninachoogopa sana kama wanawake.” Kipindi hicho alikuwa na miaka 84, mwenye chongo na aangalizia kifo.”[7]

19- ´Imraan al-Khuzaa´iy amesema:

“Sa´iyd bin al-Musayyab alisema: “Hakuna kitu nilichochelea juu ya nafsi yangu kama wanawake.” Wakasema: “Ee Abu Muhammad! Mtu kama wewe hutaki wanawake na wala wanawake hawakutaki.” Akasema: “Mambo ni kama ninavowaambieni.” Alikuwa mtumzima sana na mwenye chongo.”[8]

20- Jubayr bin Nufayr amesema:

“Umm-ud-Dardaa´ alisema kumwambia Abud-Dardaa´ wakati alipokuwa katika hali ya kukata roho: “Uliwaomba wazazi wangu katika dunia hii wanioze kwako wakakuoza. Na hivi sasa mimi nakuomba uwe mume wangu huko Aakhirah.” Akasema: “Basi usiolewe na mwingine baada yangu.” Mu´aawiyah akaja kumchumbia akamweleza yaliyopitika ambapo Mu´aawiyah akasema: “Funga.”

Imepokelewa kwa njia nyingi kupitia kwa Luqmaan bin ´Aamir ambaye ameongeza:

“Alikuwa mzuri na mrembo.”[9]

[1] 4/106.

[2] 4/126.

[3] 4/132.

[4] 4/141.

[5] 4/192.

[6] 4/233.

[7] 4/237.

[8] 4/241.

[9] 4/278.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
  • Imechapishwa: 24/12/2020