1- Abu Thawr amesema:

“ash-Shaafi´iy alikuwa mtu mwenye subira sana. Alikuwa ananunua mjakazi atakayepika na kufanya vitu tamtam. Alikuwa anamuwekea sharti ya kutofanya naye jimaa. Katika kipindi hicho alikuwa na bawasiri na hawezi kufanya jimaa na wanawake.”[1]

2- ash-Shaafi´iy amesema:

“Familia yoyote isiyowaacha wanawake zao kuolewa na wanamme wengine, au wanamme wao na wanawake wengine, isipokuwa watapata watoto wapumbavu.”[2]

3- Ahmad bin Salamah an-Naysaabuuriy amesema:

“Ishaaq bin Raahuyah alimuoa mjane wa mwanamme mmoja aliyefariki kwa sababu tu mwanamme huyo alikuwa na vitabu vya ash-Shaafi´iy. Hakumuoa kwa jengne zaidi ya vitabu.”[3]

4- Ahmad bin ´Abdillaah al-´Ijliy amesema:

“Abul-Waliyd at-Twayaalisiy kutoka Baswrah ni mwaninifu na imara katika Hadiyth. Alikuwa akipokea kutoka kwa wanawake sabini.”[4]

[1] 10/39.

[2] 10/43.

[3] 10/70.

[4] 10/344.

  • Mhusika: Imaam Shams-ud-Diyn Muhammad bin Ahmad adh-Dhahabiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Siyar A´laam-in-Nubalaa’
  • Imechapishwa: 01/02/2021