Sababu ya kuwepo makosa mengi katika “Zaad-ul-Ma´aad”

Mu´aadh (Radhiya Allaahu ´anh) amesema:

“Akianza (Swalla Allaahu ´alayhi wa salam) safari baada ya jua kupinduka, basi anaswali ´Aswr wakati wa Dhuhr.”

 Kwa hiyo inatakiwa kuyapuuza maneno ya Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) aliposema:

“Haikuwa katika uongofu wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) kukusanya swalah mbili akiwa bado yuko njiani safarini kama wanavofanya watu wengi wala kukusanya wakati amekwishatua.”[1]

Baadhi ya ndugu zetu Salafiyyuun katika baadhi ya miji wamedanganyika na maneno yake haya na ndio maana ni lazima kuwazindua.

Ni jambo la ajabu kitu kama hichi kufichikana kwa Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) kwa vile Hadiyth iko katika “al-Muwattwa´” ya Maalik na “as-Swahiyh” ya Muslim na vyenginevyo. Lakini huenda kustaajabu kukaondoka tukijua kwamba aliandika kitabu hichi “Zaad-ul-Ma´aad” akiwa safarini na akiwa hana vitabu. Hii ndio sababu ya kupatikana makosa mengi katika kitabu hicho, jambo ambalo limelibainisha katika “at-Ta´liyqaat al-Jiyaad”.

Jambo la ajabu pia ni kwamba mwalimu wake Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema waziwazi katika vitabu vyake vingi kinyume na alivosema Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah). Ni vipi hilo lilifichikana kwake kwa kuzingatia kwamba yeye ni mjuzi zaidi kumfahamu na maoni yake?

[1] Zaad-ul-Ma´aad (1/189).

  • Mhusika: Imaam Muhammad Naaswir-ud-Diyn al-Albaaniy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Silsilat-ul-Ahaadiyth as-Swahiyhah (1/1/313-314)
  • Imechapishwa: 02/05/2019