Swali: Hukumu ya mwenye kuvaa saa yenye msalaba ni haramu au inachukiza tu?

Jibu: Hapana, imekatazwa. Haijuzu. Msalaba huu ufunikwe na kitu kwa kuusugua au aweke kitu katika dawa ambayo itaufuta.

Swali: Vipi ikiwa mtu hakukusudia?

Jibu: Haijalishi kitu mtu hakukusudia. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuacha chochote chenye msalaba isipokuwa aliteketeza. Kwa hivyo saa yenye msabala ni lazima msalaba huo uondoshwe au aweke rangi itayoufuta.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/24122/حكم-لبس-ساعة-فيها-صليب
  • Imechapishwa: 02/09/2024