Swali: Ni lini mtu anaweza kuanza kwenda katika swalah ya ijumaa? Je, ni moja kwa moja baada ya swalah ya Fajr ili mtu aweze kulipwa kuwa amefika katika ile saa ya kwanza?
Jibu: Baadhi ya wanachuoni wanaonelea kuwa ile saa ya kwanza inaanza moja kwa moja baada ya swalah ya Fajr. Wengine wakasema ni baada ya jua kuchomoza. Hii ndio niliyosikia ikichaguliwa na Shaykh Ibn Baaz, ya kwamba ni baada ya jua kuchomoza.
- Muhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Sharh ´Umdat-il-Fiqh (13) http://alfawzan.af.org.sa/sites/de
- Imechapishwa: 30/09/2017
Mshirikishe mwenzako:
- Click to share on Telegram (Opens in new window) Telegram
- Click to share on WhatsApp (Opens in new window) WhatsApp
- Click to print (Opens in new window) Print
- Click to email a link to a friend (Opens in new window) Email
- Click to share on Facebook (Opens in new window) Facebook
- Click to share on X (Opens in new window) X
- Click to share on Pocket (Opens in new window) Pocket
Related
al-Fawzaan kuhusu wakati wa saa ya kwanza siku ya ijumaa
Swali: Mtu akitaka kwenda Msikitini katika ile saa ya kwanza (ambapo mtu anapata ng´ombe) ni wakati gani mtu ataenda katika nyakati za masaa ya zama zetu hizi? Ni moja kwa moja baada ya al-Fajr au ni baada ya kuchomoza kwa jua? Jibu: Yote mawili yamesemwa. Imesemekana kuwa makusudio ya “saa…
In "Swalah ya ijumaa na mengineyo yanayohusiana na ijumaa"
Ibn Baaz kuhusu wakati wa saa ya kwanza siku ya ijumaa
Swali: Ni lini inakuwa saa ya kwanza siku ya ijumaa? Jibu: Maoni yaliyo karibu zaidi na usawa ni baada ya kuchomoza jua. Baada ya kuinuka jua. Imesuniwa kwa mtu kukaa msikitini mpaka liinuke jua. Kwa hivyo maoni yaliyo karibu zaidi ni baada ya kuchomoza na kuinuka jua.
In "Swalah ya ijumaa na mengineyo yanayohusiana na ijumaa"
Nenda katika swalah ya ijumaa mapema
Swali: Aws bin Aws ath-Thaqafiy (Radhiya Allaahu ´anh) ameeleza kuwa amemsikia Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akisema: “Atakayejitwaharisha na kuoga siku ya ijumaa, akaenda kwa muda na mapema, akatembea na asipande, akawa karibu na imamu, akasikiliza na asifanye upuuzi, basi hulipwa kwa kila hatua moja ujira wa…
In "Swalah ya ijumaa na mengineyo yanayohusiana na ijumaa"