Jipime maarifa yako kuhusu wudhuu´ na swalah

Chemsha Bongo ya twahara na swalah 02

15:00

Vipi wudhuu wangu ikiwa nimeosha baadhi au viungo vyote mara mojamoja?

  • Wudhuu´ hana na lazima atawadhe tena
  • Wudhuu´ umesihi

Je, inahabika swalah ya mwenye kusoma Qur-aan kwa sauti ya juu kwenye Dhuhr na Aswr?

  • Hapana, haiharibiki amekhalifu Sunnah tu
  • Lazima arudi swalah yake

Je, vipi swalah ya mtu ambaye ana paketi ya sigara mfukoni?

  • Swalah yake inasihi
  • Hana wudhuu´ wala swalah

Je, inafaa kuswali na viatu?

  • Ndio, bali kufanya hivo ni Sunnah
  • Ndio, kwa sharti viatu viwe viapya

Ni kipi kinachotangulia kupanguswa katika Tayammum kati ya uso na viganga vya mikono?

  • Mguu
  • Viganja vya mikono

Je, inafaa kwa mtu kutawadha kwa chai au juisi ikiwa hana maji?

  • Ndio, inafaa
  • Anaweza ikiwa chai au juisi ni safi

Ikiwa mgonjwa ana udhuru wa kutoswali ikiwa amelazwa hospitali na mavazi yake saa zote ni machafu?

  • Hapana, ataswali vovyote vile kutegemea hali yake
  • Ataswali baada ya kupona

Je, inasihi swalah ya ambaye amekusudia kusoma al-Faatihah peke yake?

  • Ndio, inasihi
  • Inategemea ni faradhi au Sunnah

Je, anatakiwa kurudia wudhuu mtu anayepatwa na wasiwasi wa twahara yake mara kwa mara?

  • Ndio, anatakiwa
  • Atakiwi ikiwa amehisi maji mwilini

Je, ni lazima kuosha kila kiungo mara tatu wakati wa wudhuu?

  • Ndio, ni lazima
  • Ni lazima kwa uso tu

Je, kicheko ndani ya swalah kinaharibu swalah?

  • Ndio, kichezo kikubwa kinaharibu
  • Inafaa kucheka ndani ya swalah hapana vibaya

Je, ni ipi hukumu ya kuweka nia ya swalah kwa kutamka kwa sauti?

  • Si lazima kuweka nia kwa ajili ya swalah
  • Kuweka nia kwa kutamka kwa sauti ni Bid´ah

Je, kipi sahihi katika haya?

  • Kuwa na akili ni moja katika sharti za swalah
  • Kuwa na akili ni moja katika Sunnah za swalah

Je, inafaa imamu wa msikiti kukusanya swalah wakati wa mvua?

  • Ndio, ni Sunnah
  • Inategemea na nchi mtu anaishi

Ni ipi hukumu ya kukusudia kutosema (Rabbiy Ighfirliy) katika Rukuu?

  • Ndio, ni lazima na hivyo hana swalah
  • Inategemea hali ya mtu

Ni kipi katika haya ni nguzo mojawapo ya swalah?

  • Kuelekea Qiblah
  • Kusoma al-Faatihah

Je, swalah ya mtu aliyesahau kuketi kati ya sujuud mbili imeharibika?

  • Ndio, imeharibika
  • Inategemea ni swalah ya faradhi au ya sunnah

Je, swalah ya mtu inabatilika akiacha kusoma al-Faatihah kwa kusahau?

  • Ndio, inabatilika na lazima aswali tena
  • Inategemea ikiwa ni swalah ya faradhi au sunnah

Je, anakufuru mwenye kuacha kuswali makusudi?

  • Ndio, sahihi ni kwamba anakufuru
  • Hakufuru kama ni muislamu safi

Ni kipi katika haya ni sahihi?

  • Zote zinalingana
  • Swalah ya aliyepiga Siwaak ni bora zaidi ikiwa ni ya faradhi tu na si ya Sunnah

Je, inafaa kwa mtu kuswali huku amevaa nguo chafu lakini si najisi?

  • Hapana, haifai
  • Inafaa tu ikiwa hana nguo nyingine

Ni ipi hukumu ya kuswali huku unahisi haja kubwa au ndogo?

  • Inategemea muda wa swalah
  • Ni jambo linalochukiza na swalah inafaa