Jipime maarifa yako kuhusu twahara na swalah
Chemsha Bongo ya twahara na swalah 14
15:00
Ni ipi hukumu ya anayeswali faradhi kwa kuketi ilihali anaweza kusimama?
- Kusimama kwa anayeweza ni mojawapo ya sharti za swalah na hivyo anatakiwa kuirudia swalah yake
- Inafaa kuswali kwa kukaa chini na si lazima kusimama
- Inafaa kwake kusimama katika zile Rak'ah 2 za mwisho peke yake
Ni kipi katika haya ni mojawapo ya sharti za swalah?
- Kusoma al-Faatihah
- Kunyoosha kidole katika Tashahhud
- Kuondosha hadathi (kutawadha)
Ni ipi hukumu ya anayeswali na makalio yake yanaonekana wakati wa kusujudu na kurukuu?
- Hapana vibaya muhimu aswali
- Inafaa kama ni swalah ya Sunnah na si swalah ya faradhi
- Kufunika uchi ni mojawapo ya sharti za swalah na hivyo kunakhofiwa swalah yake isikubaliwe
Je, maamuma warudie swalah ya imamu ambaye baada ya swalah amekumbuka hakutawadha?
- Ndio
- Hapana, lakini ni lazima kwa imamu kuirudia
- Maamuma ndio watarudia na si maamuma
Ni kipi kilichosihi katika haya?
- Swalah ndio nguzo ya Uislamu
- Swalah bora kwa mwanaume ni nyumbani kwake
- Swalah ndio nguzo ya Uislamu
Ni ipi hukumu ya mwanaume kuswali na suruwali?
- Inafaa muhimu iwe pana na yenye kusitiri
- Haifai na swalah haisihi
- Vazi pekee la swalah ni kanzu
Je, maamuma warudie swalah ya imamu ambaye baada ya swalah amekumbuka ameswali na nguo najisi?
- Hapana, si imamu wala maamuma hawatoirudia
- Ndio, wairudie wote
- Imamu tu ndiye atarudia na si maamuma
Ni kipi kilichosihi katika haya?
- Swalah bora ya mwanamke ni kwenye msikiti wa Makkah
- Swalah bora ya mwanamke ni nyumbani kwake
- Swalah bora ya mwanamke ni akiwa amejisitiri
Ni ipi hukumu ya kuswali shambani na vipi kuhusu usafi wake?
- Haifai kwa.s si kusafi
- Akiswali swalah haisihi
- Inafaa kwa.s msingi ni kufaa kuswali maeneo kote
Ni kipi katika haya ni mojawapo ya nguzo za swalah?
- Kugeuka kuliani na kushotoni wakati wa kutoa salamu
- Kufikisha miaka ya kupambanua
- Kuangalia mahali pa kusujudia
Ni ipi hukumu ya kuswali na nguo za kazi zilizo chafu?
- Haifai na swalah haisihi
- Swalah inakuwa na nguo safi tu
- Inafaa muhimu zisiwe na najisi
Ni ipi hukumu ya mfungwa ambaye mahali alipofungwa ni najisi na hana ruhusa ya kutoka nje kuswali?
- Asiswali yuko na udhuru
- Akiswali swalah haikubaliwi
- Aswali kwa hali yoyote na si ruhusa kwake kuacha swalah
Ni ipi hukumu ya anayeswali bila ya kukimu swalah?
- Inafaa kukimu si lazima
- Lazima kukimu na sivyo swalah haisihi
- Lazima kukimu na la sivyo swalah ina mapungufu
Ni ipi hukumu ya anayekosa swalah tatu za ijumaa kwa mfululizo?
- Haina neno kama ni kwa.s ya kazi
- Allaah ataupiga muhuri moyo wake
- Amekufuru
Ni ipi hukumu ya msichana kuswali kichwa wazi?
- Inafaa na haina neno
- Kama ameshabaleghe swalah haisihi
- Inafaa kuswali namna hiyo katika swalah ya Sunnah peke yake
Je, inafaa kupangusa juu ya viatu?
- Ndio, kama vinafunika macho mawili ya miguu
- Haifai hayo ni matendo ya makafiri
- Akifanya hivo swalah haisihi
Ni ipi hukumu ya swalah ya mswaliji asiyenyanyua mikono juu wakati wa Takbiyrat-ul-Ihraam?
- Hana swalah, kwa.s Takbiyrat-ul-Ihraam ni nguzo
- Swalah yake inasihi muhimu aitamke
- Ni nguzo kunyanyua tu katika swalah za faradhi na si za Sunnah
Ni ipi hukumu ya mwanaume kuswali na mavazi ya kubana?
- Swalah haisihi
- Haipendezi na ni lazima vazi la swalah lifunike viungo visivyotakiwa kuonekana
- Inafaa kwa mwanaume na si kwa mwanamke
Imesuniwa kwa mwanamke anayeswali peke yake kutoa adhaana na kukimu kwa ajili ya kuswali?
- Ndio, ni Sunnah ya lazima
- Hapana, ni jambo maalum kwa wanaume
- Lazima kwa mwanamke kabla ya kuswali aadhini na kukimu
Ni lini mtu anazingatiwa ameiwahi swalah ya ijumaa?
- Atakapowahi Rukuu´ katika Rak´ah ya pili
- Atakapowahi Sujuud katika Rak´ah ya pili
- Atakapowahi Tashahhud katika Rak´ah ya pili
Ni nani katika hawa ana haki zaidi ya kutoa adhaana?
- Aliyejenga msikiti
- Ambaye ana uwezo wa kuhudhuria kila swalah
- Ambaye ana sauti kubwa inayofika mbali zaidi
Ni kipi kilichosihi katika haya kuhusu swalah ya Mtume?
- Swalini kama mlivyoniona ninaswali
- Swalah ni bora kuliko chakula
- Swalah ndio ufumbuzi wa kila tatizo