Jipime maarifa yako kuhusu twahara na swalah
Chemsha Bongo ya twahara na swalah 12
15:00
Ni nani ana haki zaidi ya kumswalia maiti?
- Ambaye maiti kaacha anausia
- Mume au mke
- Mzazi wa maiti
Mtu anatumia mkono gani wakati wa kupenga?
- Kulia
- Kushoto
- Mkono wowote
Vipi twahara ya mwanamke aliyepaka rangi ya kucha inayozuia maji kufika kwenye kucha?
- Inasihi
- Ni sawa ni kama hina
- Haisihi
Je, inafaa kutumia maji ya zamzam kwa ajili ya kutamba?
- Unapata dhambi kwa kuyatumia
- Inafaa tu kama choo ni kisafi
- Sahihi ni kwamba inafaa
Ni Suurah ipi inayosema swalah inamzuia mtu kutokana na machafu na maovu?
- al-Baqarah
- al-'Ankabuut
- al-Faatihah
Ni usingizi upi unachengua wudhuu?
- Usingizi wote
- Usingizi ambao mtu hajui kinachoendelea kando na yeye
- Usingizi hauchengui wudhuu', kulala tu ndio kunachengua
Ni msafiri wa siku ngapi anazingatiwa na kuruhusiwa kufupisha swalah?
- Salama zaidi ni safari isiyozidi siku 4
- Safari yoyote anaruhusiwa kufupisha swalah
- Ni ile safari isiyozidi siku 100
Sunnah na bora mtu afanye Adhkaar kwa mkono wa kuume au kushoto au yote miwili?
- Yote miwili
- Bora ni kufanya kwa mkono wa kuume
- Mkono wa kushoto
Je, inafaa mara kwa mara kukusanya kati ya Maghrib na Ishaa mchana unapokuwa mrefu na kesho mtu ataamkia kazini au shuleni?
- Hapana, haifai
- Ndio, inafaa hiyo ni dharura
- Inafaa tu kwa wafanyakazi kukusanya
Je, inafaa kumswalia maiti ambaye alikuwa haswali kabisa?
- Sahihi ni kwamba haifai kwa.s ni kafiri
- Ndio, inafaa kwa.s ni faradhi ya kutosheleza
- Inafaa lakini usimwombei du'aa ya msamaha na rehema
Je, inafaa kwa msafiri kukusanya kati ya Ijumaa na Aswr?
- Ndio, bali inapendeza
- Sahihi ni kwamba haifai
- Hapana, ni haramu
Ni lazima kuelekea Qiblah wakati wa kutawadha?
- Ndio, ukikusudia kukipa Qiblah mgongo wudhuu' hausihi
- Si lazima
- Hapana, ila tu kama ni wudhuu' wa kufanyia 'ibaadah ya wajibu
Swalah ya faradhi inasihi juu ya kipando kwa kukaa?
- Ndio, hapana vibaya
- Haisihi kama ameweza kusimama akaacha kufanya hivo, kwani kusimama ni nguzo ya swalah
- Ana khiyari ya kusimama na kukaa
Mtu aliyekosa Dhuhr na umefika wakati wa Aswr, anaanza na swalah gani?
- Ataanza Dhuhr kisha ´Aswr
- Ataanza 'Aswr kisha Dhuhr
- Ataanza yoyote muhimu aswali zote
Ni nyama ya mnyama upi inachengua wudhuu katika hizi?
- Kenge
- Farasi
- Ngamia
Ni ipi hukumu ya mazowea watu kupeana mkono (kusalimiana) baada ya kumaliza swalah ya mkusanyiko msikitini?
- Ni Sunnah kufanya hivo
- Ni jambo halina msingi khasa kama walisalimiana kabla ya swalah
- Wanapeana mkono wanasamehewa dhambi zao
Kabla ya kuanza swalah unatakiwa kuhakikisha umeondosha najisi sehemu tatu. Ni zipi?
- Mahali unaposwalia, nguo zako na mavazi yako
- Mahali unaposujudia, unapoelekea na nguo yako ya ndani
- Kwenye mkeka wako, nyumba yako na msikitini
Ni ipi hukumu ya kutumia maji ya bwawa au mto ambayo mtu hajui usafi wake?
- Ni lazima uwe na uhakika kuwa ni safi vinginevyo haifai kuyatumia
- Maji aina hiyo ni najisi
- Msingi wa maji yote ni safi mpaka ithibiti kinyume chake
Je, inafaa kushika utupu kwa mkono wa kulia?
- Ndio, hapana vibaya
- Ashike tu baadhi ya nyakati
- Hapana, haifai
Ni ipi hukumu ya kuswali na nguo yangu iliyopatwa na mkojo wa kondoo au mbuzi?
- Lazima kuifua kwa.s ni najisi
- Mkojo wa kila mnyama anayeliwa si najisi
- Ni najisi na hivyo lazima atafute nguo nyingine
Ni ipi hukumu ya kusoma Basmalah kwa sauti mwanzoni mwa Suurah ndani ya swalah?
- Ni lazima la sivyo swalah haisihi
- Ni lazima katika swalah za faradhi
- Sunnah ni kusoma kimyakimya, lakini hapana vibaya kusoma kwa sauti baadhi ya nyakati
Ni ipi hukumu ya kupitisha maji kati ya vidole vya miguu wakati wa kutawadha?
- Si jambo la lazima
- Ni lazima maji yaingie ndani ya vidole vyote
- Ni khiyari ya mtu