Jipime maarifa yako kuhusu twahara na swalah
Chemsha Bongo ya twahara na swalah 11
15:00
Ni ipi hukumu ya kufanya Tawarruk?
- Ni Sunnah
- Hakuna kitu hicho
- Ni lazima la sivyo swalah haisihi
Swalah ya jeneza ina Takbiyr ngapi?
- 7
- 5
- 4
Ni Sunnah kusoma Suurah zipi katika swalah ya Fajr siku ya ijumaa?
- Aayat-ul-Kursiy na al-Insaan
- as-Sajdah na al-Insaan
- as-Sajdah na al-Mulk
Je, aje kuswali msikitini ambaye ananuka vitunguu saumu na vitunguu maji?
- Ndio, aje na hana udhuru wa kuacha swalah ya mkusanyiko
- Akiswali nyumbani anapata dhambi
- Ana udhuru wa kuswali nyumbani maadamu hajakusudia kukwepa swalah ya mkusanyiko
Ni ipi hukumu ya kukimbia msikitini kwa ajili ya kuwahi Rakah?
- Ni jambo limekatazwa
- Haifai kama tu ni swalah ya faradhi
- Hapana ubaya wowote kufanya hivo
Vipi wudhuu wa ambaye amegusa au amekanyaga kinyesi au mkojo?
- Bado yuko na wudhuu´ wake
- Wudhuu´ wake anaweza kuuswalia swalah za sunnah
- Umechenguka
Ni ipi hukumu ya anayekusanya swalah zaidi ya moja wakati anaporudi kutoka kazini?
- Ni sawa kwani kazi pia ni 'ibaadah
- Sahihi ni kwamba swalah zake hazikubaliwi na kunakhofiwa juu yake ukafiri
- Swalah zake zinasihi na hapana vibaya
Je, inafaa kuswali kwenye udongo, mchanga au nyasi ambazo mtu hajui usafi wake?
- Hapana, haifai
- Swalah haisihi ila kwenye mkeka tu
- Msingi wa ardhi yote ni safi na hivyo inasihi
Ni yepi malipo ya anayetembea kwa miguu kwenda msikitini?
- Ana malipo 40 kwa kila hatua anayopiga
- Anafutiwa madhambi 10 kwa kila hatua anayopiga
- Kwa kila hatua anafutiwa kosa na kupandishwa daraja
Ni ipi hukumu ya kuomba kinga dhidi ya shaytwaan kabla ya kusoma Suurah na ni katika kila Rakah?
- Ni jambo la wajibu, lakini ni katika Rak'ah ya kwanza tu
- Ni katika kila Rak'ah na hana swalah asipofanya hivo
- Ni lazima kwa imamu tu na si maamuma
Ni ipi hukumu ya mwanaume kufunika kichwa wakati wa kuswali?
- Inapendeza, ni katika utimilifu wa swalah
- Ni wajibu la swalah haisihi
- Ni katika masharti ya kukubaliwa swalah
Ni ipi hukumu ya kuomba kinga dhidi ya shaytwaan wakati wa kuswali na ni lini?
- Ni wajibu, inakuwa baada ya du'aa ya kufungulia swalah na kabla ya Basmalah
- Ni Sunah, inakuwa kabla ya du'aa ya kufungulia swalah na kabla ya Basmalah
- Ni nguzo ya swalah na swalah haisihi mtu akiiacha
Ni ipi hukumu ya kurukuu kabla ya kufika kwenye safu kwa ajili ya kuwahi Rakah?
- Imekatazwa kufanya hivo
- Ni sawa kwa.s ni kupupia katika mambo ya kheri
- Inafaa kwa.s Swahabah Abu Bakrah alifanya hivo
Nini anachofanya mtu ambaye amepitwa na swalah ya jeneza nyumbani kwa maiti au msikitini?
- Ataenda kumswalia makaburini
- Ameshaikosa na hakuna namna
- Ataenda kumswalia makaburini kama tu ni Shaykh au mtu mwema
Je, inafaa kuswali nyuma ya muislamu ambaye mtu hajui itikadi yake?
- Ndio, msingi ni kwamba kunaswaliwa nyuma ya kila muislamu
- Hapana, usiswali nyuma ya mtu mpaka ujue itikadi yake
- Inafaa tu kuswali nyuma yake kama ni mtawala wa kiislamu
Ni ipi hukumu ya mtu kutilia shaka swalah yake baada ya kumaliza?
- Shaka baada ya kumaliza 'ibaadah haizingatiwi
- Airudi swalah yake
- Atawadhe na aswali tena kwa unyenyekevu
Nifanye nini wakati imamu anaporukuu na sijamaliza kusoma al-Faatihah?
- Lazima umalize kuisoma
- Simama ulipoishilia na umfuate imamu
- Swalah yako haisihi na lazima uswali tena
Ni ipi hukumu ya kufanya nyuradi kwa pete ya kidole?
- Sunnah
- Bid'ah
- Ni kama Subha na hivyo haina neno
Ni ipi hukumu imamu kuchanganya visomo vingi (katika vile visomo 7) katika swalah moja?
- Haina neno maadamu vimethibiti
- Ni kuhuisha Sunnah na hivyo imehimizwa
- Inachukiza kufanya hivo kwani inawashawishi waswaliji
Je, kuna Dhikr maalum inayosomwa wakati wa sujuud ya kisomo?
- Ndio, ipo
- Hapana hakuna. Atasema "Subhaana Rabbiyal A'laa
- Atasema 'Rabbana walakal hamd"
Je, inafaa kwa mwanamke kumswalia maiti?
- Hapana, wanaume tu
- Inafaa lakini nyumbani kwake tu
- Ndio, inafaa nyumbani na msikitini
Ni swalah ipi katika hizi isiyokuwa na Rukuu wala Sujuud?
- Istisqaa'
- Swalah ya jeneza
- Kusuuf