Jipime maarifa yako kuhusu twahara na swalah
Chemsha Bongo ya twahara na swalah 06
15:00
Ni kipi katika haya ni mojawapo ya nguzo za swalah?
- Tashahhud ya kwanza
- Kusema "Allaahu Akbar"
- Kusema "Aamiyn"
Nini anachotakiwa kufanya aliyepitiwa na usingizi na akaamka wakati jua linapozama?
- Atasubiri jua lizame
- Atasubiri mpaka wakati wa Ishaa
- Ataswali Dhuhr papohapo
Ni ipi hukumu ya swalah ya aliyesahau kusema (Subhaana Rabbiyal Aalaa)?
- Atasujudu sijda ya kusahau kama muda haujarefuka
- Hana swalah lazima airudie
- Atasema tu kilichompita na swalah imesihi
Nini anachotakiwa kufanya aliyepitiwa na usingizi na akaamka wakati jua linapochomoza?
- Atasubiri jua lichomoze
- Ataswali Far papohapo
- Atasubiri mpaka wakati wa Dhuhaa
Ni ipi hukumu ya kuswali ndani ya msikiti wenye kaburi?
- Swalah haisihi na lazima irudiwe
- Swalah inasihi tu kama ni kaburi la Mtume
- Swalah ina mapungufu lakini inasihi
Nini afanye mtu ambaye anataka kufanya tendo la ndoa na hakuna maji au anayo maji madogo ya kumtosha kunywa tu?
- Lazima asubiri mpaka kupatikane maji
- Akifanya na anajua hakuna maji anapata dhambi
- Afanye kisha atafanya Tayammum
Ni ipi hukumu ya kuswali Sunnah wakati jua linapinduka (Takrian dakika 20 kabla ya kuingia Dhuhr)?
- Inafaa haina neno
- Imekatazwa
- Inafaa kuswali Dhuhaa peke yake
Ni lini watoto huanza kupigwa wanapokataa kuswali?
- Miaka 7
- Miaka 5
- Miaka 10
Ni kweli kwamba muda wa swalah ya usiku inaanza baada ya Maghrib?
- Hapana, ila kwa msafiri tu
- Ndio, katika baadhi ya hali
- Unaanza baada ya 'Ishaa katika hali zote
Ni ipi hukumu ya swalah ya aliyesahau kusema (Subhaana Rabbiyal Adhwiym)?
- Lazima airudi swalah yake
- Kama hakujapita kitambo kirefu atasujudu sijda ya kusahau
- Ataswali swalah nyingine badala yake
Je, inafaa kwa mwanamke kuswali miguu wazi?
- Ndio, haina neno
- Hapana, haifai
- Inafaa tu kama hakuna wanaume wanaomuona
Ni ipi hukumu ya swalah ya mtu aliyeswali ndani ya msikiti wenye kaburi miaka 2 iliyopita?
- Hakuna kinachomlazimu hakuwa anajua
- Swalah inasihi japo ana madhambi
- Swalah haisihi na lazima aurudie
Kwanini ikakatazwa kuswali Sunnah wakati jua linapochomoza?
- Kwa.s wakati wake unakuwa hujaingia
- Kwa.s jua linakuwa kali
- Ni kujifananisha na waabudia jua
Kwanini imekatazwa kuswali Sunnah wakati jua linapozama?
- Kwa.s jua linakuwa na madhara
- Ni kujifananisha na waabudia jua
- Kwa.s wakati wake unakuwa umeshapita
Je, inafaa kuswali swalah nyingi kwa twahara ya Tayammum?
- Hapana
- Ndio
- Inafaa tu kama ni msafiri
Kwanini ikakatazwa kutamba kwa mifupa?
- Kwa.s ni chakula cha ndugu zetu majini na pia haisafishi
- Kwa.s inaumiza
- Kwa.s ni ina madhara kwenye utupu
Kama imekatazwa kuswali kwa kuliekea kaburi kwanini swalah ya jeneza tunaliekea kaburi na maiti?
- Haifai kufanya hivo
- Inachukiza kufanya hivo
- Kwa.s malengo ni kumuombea maiti na jengine ni swalah isiyo na Rukuu´ wala Sujuud
Mtu anatakiwa ajisafishe utupu wake kwa mawe yasiyopungua mangapi?
- 3
- 5
- 2
Ni ipi hukumu ya kuswali kwa kulielekea kaburi?
- Swalah inasihi lakini ina mapungufu
- Ni haramu na swalah haisihi
- Haina neno na swalah inasihi
Ni viungo vingapi katika wudhuu lazima vioshwe na ni vipi?
- 3, kusukutua mdomo, kupangusa kichwa na kuosha miguu
- 2, kuosha mikono na miguu
- 4, kuosha nyuso, mikono mpaka kwenye visugudi, panguseni vichwa na kuosha miguu hadi vifundoni
Inafaa kujisafisha ufupu kwa mifupa?
- Ndio, inafaa
- Haifai
- Inafaa tu wakati umekosa mawe
Ni vipi mwanamke anamzindua imamu anayekosea katika kisomo cha Qur-aan?
- Kwa kutamka kwa sauti
- Kwa kusema "Subhaanallaah"
- Kwa kupiga makofi