Jipime maarifa yako kuhusu siku na swalah ya idi

Chemsha Bongo siku na swalah ya idi 02

08:20

Kwanini inasuniwa kuharakisha swalah ya idi Adhwhaa?

  • Ili watu waende kusalimia jamaa zao
  • Ili watu wawahi kwenda kuchinja baada ya swalah

Kuna tamko maalum la kupongezena lililothibiti kwa ajili ya idi?

  • Hapana, mtu anaweza kutumia tamko lolote
  • Ndio, imethibiti kwa Salaf

Je, inafaa kupiga dufu siku ya idi na linapigwa na nani?

  • Hapana, ni haramu kwa hali yoyote
  • Ndio, watoto wa kike tu

Ni ngapi Takbiyr za swalah ya idi Fitwr Rakah ya kwanza?

  • Ni 7 baada ya Takbiyrat-ul-Ihraam
  • Ni 5 baada ya Takbiyrat-ul-Ihraam

Kipi kilichosihi katika haya?

  • Imesuniwa kula baada ya kuswali idi al-Adhwhaa
  • Imesuniwa kutokata kucha kabla ya swalah ya idi al-Fitwr

Ni lini unalazimika muda wa kuswali swalah ya idi mbili?

  • Takriban dakika 15 baada ya jua kupondoka
  • Kabla ya kufika muda wa alasiri

Sherehe ya idi al-Fitwr inakuwa siku ngapi?

  • Siku tatu
  • Siku nne

Ni lini inamalizika Takbiyr ya idi Fitwr?

  • Baada ya kuzama jua siku ya nne
  • Baada ya kuzama jua ile siku ya kwanza ya idi

Vipi swalah ya idi ikiwa watu wamejua kuwa ni siku ya idi baada ya kuwa jua limeshapinduka?

  • Badala ya swalah ya idi wataswali Dhuhr
  • Watu wataswali kesho hali ya kuilipa

Je, kumethibiti Dhikr maalum ya kusoma baina ya zile Takbiyr 7 na 5 za idi?

  • Hapana akae kimya, ila imepokelewa kwamba baadhi ya Salaf walikuwa wakileta Dhikr
  • Ndio, inasomwa Dhikr kama kwenye Rukuu'

Ni kipi kilichosihi katika haya?

  • Imesuniwa kula tende kabla ya kwenda kuswali 'Iyd-ul-Fitwr
  • Ni wajibu kutoa swadaqah kabla ya kwenda kuswali idi