Pindi namna ya vazi linapoenda sambamba na Sunnah

Swali: Ni lini vazi linakuwa la umashuhuri?

Jibu: Mtu anapotofautiana na watu wa mji wake katika mavazi yao. Haijalishi kitu katika uzuri au ubaya, nguo iliochanika au linaloenda kinyume na mavazi yao katika kuwa kwake na bei kubwa na umashuhuri.

Swali: Wako wanaosema kuwa ni umashuhuri ikiwa inafika katika nusu muundi?

Jibu: Kuvaa nusu muundi hakuitwi kuwa ni mavazi, hilo ni katika namna. Asijali yanayofanywa na watu pale ambapo namna ya vazi inaafikiana na Sunnah.

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23292/متى-يكون-اللباس-لباس-شهرة
  • Imechapishwa: 21/12/2023