Picha zilizohifadhiwa na masanamu ya mapambo

Swali: Je, ni haramu kutundika picha ya mtu au ya mnyama nyumbani? Ni ipi hukumu ya masanamu nyumbani kama mapambo?

Jibu: Ndio, kutundika picha ukutani ni haramu na haijuzu. Ambaye ametundika picha yoyote ni lazima kwake kuiondosha na aichome moto. Haijuzu kuihifadhi kwenye albamu, sanduku wala mahali kwengine kokote. Kwa sababu kuhifadhi picha haijuzu. Hakuna picha iliyoruhusiwa isipokuwa ile inayotwezwa, kama vile picha za kwenye mazulia na mito – licha ya kwamba kuna tofauti juu ya hilo pia.

Kuhusu masanamu yenye umbile la mtu na mnyama, ni jambo kubwa na baya zaidi. Ni wajibu kuyaharibu au angalau kwa uchache yakatwe vichwa vyake. Nashangazwa na watu ambao wanayaweka mbele ya nyumba zao na hivyo wanakuwa ni wenye kuwazuia Malaika kuingia nyumbani zao. Kwa ajili hiyo ´Aliy (Radhiya Allaahu ´anh) amesema kumwambia Abul-Hayyaaj:

“Hivi nisikutume juu ya kazi aliyonituma kwayo Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam)? Usiache picha hata moja isipokuwa umeiharibu wala kaburi lililoinuka isipokuwa umelisawazisha.”[1]

[1] Muslim (969).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/353)
  • Imechapishwa: 09/04/2026