Swali: Mtu aliyeingia katika swalah pamoja na imamu huenda ikatokea katika Rak´ah ya tatu au nyingine kwamba imamu anarukuu kabla hajamaliza kusoma al-Faatihah. Je, achelewe nyuma ya imamu ili amalize kuisoma au arukuu pamoja na imamu kisha ailipie Rak´ah hiyo au hukumu yake ni kama ya aliyemkuta imamu akiwa tayari katika Rukuu´ na hakuna chochote juu yake?
Jibu: Anatakiwa ajitahidi aisome kabla imamu hajarukuu. Anatakiwa ajitahidi na asifanye uzembe, bali ajitahidi kuisoma kabla imamu hajarukuu. Ikiwa imamu atarukuu na yeye amebakiwa na Aayah moja au mbili, basi aimalizie kisha arukuu, kwani hakuna kinachomzuia kuimalizia kisha akaenda katika Rukuu´. Lakini ikiwa anaogopa kwamba Rukuu´ itampita, basi aikatize, alete Takbiyr na arukuu pamoja na imamu. Katika hali hiyo anakuwa na udhuru.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/152)
- Imechapishwa: 06/03/2026
Swali: Mtu aliyeingia katika swalah pamoja na imamu huenda ikatokea katika Rak´ah ya tatu au nyingine kwamba imamu anarukuu kabla hajamaliza kusoma al-Faatihah. Je, achelewe nyuma ya imamu ili amalize kuisoma au arukuu pamoja na imamu kisha ailipie Rak´ah hiyo au hukumu yake ni kama ya aliyemkuta imamu akiwa tayari katika Rukuu´ na hakuna chochote juu yake?
Jibu: Anatakiwa ajitahidi aisome kabla imamu hajarukuu. Anatakiwa ajitahidi na asifanye uzembe, bali ajitahidi kuisoma kabla imamu hajarukuu. Ikiwa imamu atarukuu na yeye amebakiwa na Aayah moja au mbili, basi aimalizie kisha arukuu, kwani hakuna kinachomzuia kuimalizia kisha akaenda katika Rukuu´. Lakini ikiwa anaogopa kwamba Rukuu´ itampita, basi aikatize, alete Takbiyr na arukuu pamoja na imamu. Katika hali hiyo anakuwa na udhuru.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/152)
Imechapishwa: 06/03/2026
https://firqatunnajia.com/nimalize-al-faatihah-au-niikatishe-na-kurukuu-pamoja-na-imamu/