Nifanye Tayammum au nisubiri mpaka nifike katika mji ninapoenda?

Swali: Ikiwa niko safarini na muda wa swalah ya Dhuhr umeingia, lakini sina maji ya kutawadhia. Kati yangu na mji ulio mbele yangu kuna takriban saa mbili au tatu za safari, kiasi kwamba nitafika mjini kabla ya muda wa Dhuhr kuisha, je, nifanye Tayammum na kuswali au nisubiri mpaka nifike mjini?

Jibu: Muda wa swalah unapoingia, basi ni wajibu kwa mwenye kupewa jukumu la Shari´ah kutafuta maji. Asipopata maji, basi afanye Tayammum na kuswali. Asisubiri kufika katika mji ulio mbele yake. Isipokuwa ikiwa anaendelea na safari yake na ana uhakika wa kufika mjini, basi inajuzu kwake kuchelewesha swalah mpaka mwisho wa wakati wake.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/343)
  • Imechapishwa: 22/11/2026