Tayammum moja kwa ajili ya faradhi zote au Tayammum kwa kila swalah?

Swali: Ikiwa msafiri anafupisha swalah na anafanya Tayammum, je, inajuzu kwake kufanya Tayammum moja kwa swalah zote za faradhi au ni lazima afanye Tayammum kwa kila swalah?

Jibu: Inamtosheleza kufanya Tayammum moja kwa ajili ya kuswali zaidi ya swalah moja ya faradhi au faradhi moja na swalah ya Sunnah, muda wa kuwa bado yuko katika hali ya twahara na hajapata maji. Haya ndiyo maoni sahihi miongoni mwa maoni mawili ya wanazuoni.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/344)
  • Imechapishwa: 22/11/2026