Ni wapi anaposimama anayemuombea maiti kaburini?

Swali: Je, mtu anapozuru kaburi, anatakiwa akielekee Qiblah?

Jibu: Kilicho bora ni kusimama upande wa uso wa aliyekufa kama ikiwezekana, si lazima kuelekea Qiblah. Bora ni kusimama mbele ya uso wake kama vile ungemtembelea akiwa hai na ungekuwa ukimkabili. Hii ndiyo njia nzuri zaidi ikiwa inawezekana. Lakini ikiwa haitawezekana, basi simama upande wowote utoe salamu na inatosha. Hata kama utapita kati ya makaburi, ukawapa wote sakamu kisha ukaendelea na safari yako, inatosha.

Swali: Vipi kama ninataka kumuombea du´aa?

Jibu: Mwombee du´aa na wewe huku ukitembea.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/1126/هل-استقبال-القبلة-شرط-عند-زيارة-القبر
  • Imechapishwa: 30/01/2026