Ni msafiri anayeenda umbali wa 100 km nje ya mji wake?

Swali: Mtu anaposafiri umbali wa 100 km kwenda katika mji fulani, je, inafaa kwake kukusanya na kufupisha swalah?

Jibu: Mtu anaposafiri kutoka katika mji wake umbali wa 100 km au unaokaribia hapo, basi anatumia hukumu za safari katika kupunguza swalah, kufungua, kukusanya swalah mbili na kupaka juu ya soksi za ngozi kwa muda wa siku tatu, kwa sababu umbali huu unahesabiwa kuwa ni safari.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (30/181)
  • Imechapishwa: 09/03/2026