Ni lini mtu anamswalia Mtume katika adhaana?

Swali: Baada ya shahaadah mbili kuna upokezi  unaosema kwamba mtu anatakiwa kusema:

“Na mimi nashuhudia kuwa kuwa hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah. Nimeridhika na Allaah kama Mola…”?

Jibu: Hayo yanasemwa wakati wa shahaadah mbili, anatakiwa kusema mfano wake, kama alivyopokea Sa´d bin Abiy Waqqaaas:

“Mtu yeyote atakayesema wakati muadhini anaposema: ”Nashuhudia ya kuwa hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah…” kisha akasema: ”Nimeridhika na Allaah kuwa Mola wangu, Uislamu dini yangu na Muhammad Mtume wangu.”,

basi atasamehewa madhambi yake.”

Swali: Vipi kuhusu upokezi unaosema:

”Na mimi nashuhudia ya kuwa hapana mungu wa haki isipokuwa Allaah…”?

Jibu: Maana ni moja. Ni mamoja atasema:

“Nashuhudia…”

au:

“Nami nashuhudia… ”,

kwa sababu riwaya zimekuja kwa matamshi tofauti.

Swali: Lakini upande wa mapokezi ni Swahiyh?

Jibu: Dhahiri ni kwamba ni Swahiyh. Ikiwa mtu atasema:

“Nashuhudia ya kuwa hakuna mungu wa haki isipkuwa Allaah… ” au akasema “Na mimi nashuhudia ya kuwa hakuna mungu wa haki isipokuwa Allaah… ”,

basi atakuwa amesema mfano wake.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/27329/متى-يقال-وانا-اشهد-في-ترديد-الاذان
  • Imechapishwa: 23/03/2025