Ni lini inafaa kumjamii mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi?

Swali: Ni lini inafaa kumjamii mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi?

Jibu: Haijuzu kuwajamii mwanamke mwenye hedhi na mwenye damu ya uzazi isipokuwa baada ya kumalizika hedhi au damu ya uzazi na wakaoga. Amesema (Ta´ala):

وَلَا تَقْرَبُوهُنَّ حَتَّىٰ يَطْهُرْنَ ۖ فَإِذَا تَطَهَّرْنَ فَأْتُوهُنَّ مِنْ حَيْثُ أَمَرَكُمُ اللَّـهُ

“Wala msiwakaribie kujimai nao mpaka watwaharike. Watakapotwaharika basi waendeeni kupitia pale alipokuamrisheni Allaah.”[1]

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz

Swaalih al-Fawzaan

´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah Aalish-Shaykh

Bakr bin ´Abdillaah Abu Zayd

[1] 02:222

  • Mhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Lajnah ad-Daaimah nr. (17332)
  • Imechapishwa: 09/06/2022