Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth kuhusu saa ya kujibiwa du´aa siku ya ijumaa:
“… naye akiwa amesimama akiswali.”
Je, hii ina maana kwamba mtu akitaka kuomba du´aa ni lazima awe ndani ya swalah?
Jibu: Hapana, si lazima. Kuhusu saa ya ijumaa, wanazuoni wametofautiana kuhusu wakati wake kwa maoni mengi. Haafidhw Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) amesema:
”Wanazuoni wametofautiana kuhusu saa hiyo kwa maoni arobaini. Lakini maoni yenye nguvu zaidi ni mawili:
1 – Ni kuanzia wakati Khatwiyb anapoingia siku ya ijumaa hadi swalah inapomalizika. Hivyo mtu huomba du´aa katika vipindi vya unyamazo wa imamu, baina ya Khutbah mbili, katika Sujuud na ndani ya swalah.
2 – Ni saa ya mwisho ya siku ya ijumaa baada ya ´Aswr.
Zimekuja Hadiyth kuhusu jambo hili.
Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“… naye akiwa amesimama akiswali.”
haimaanishi kuwa ni lazima awe anaswali, kwa sababu anayengojea swalah anahesabiwa kuwa yuko katika hukumu ya mwenye kuswali.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
- Imechapishwa: 18/09/2026
Swali: Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema katika Hadiyth kuhusu saa ya kujibiwa du´aa siku ya ijumaa:
“… naye akiwa amesimama akiswali.”
Je, hii ina maana kwamba mtu akitaka kuomba du´aa ni lazima awe ndani ya swalah?
Jibu: Hapana, si lazima. Kuhusu saa ya ijumaa, wanazuoni wametofautiana kuhusu wakati wake kwa maoni mengi. Haafidhw Ibn Hajar (Rahimahu Allaah) amesema:
”Wanazuoni wametofautiana kuhusu saa hiyo kwa maoni arobaini. Lakini maoni yenye nguvu zaidi ni mawili:
1 – Ni kuanzia wakati Khatwiyb anapoingia siku ya ijumaa hadi swalah inapomalizika. Hivyo mtu huomba du´aa katika vipindi vya unyamazo wa imamu, baina ya Khutbah mbili, katika Sujuud na ndani ya swalah.
2 – Ni saa ya mwisho ya siku ya ijumaa baada ya ´Aswr.
Zimekuja Hadiyth kuhusu jambo hili.
Maneno yake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“… naye akiwa amesimama akiswali.”
haimaanishi kuwa ni lazima awe anaswali, kwa sababu anayengojea swalah anahesabiwa kuwa yuko katika hukumu ya mwenye kuswali.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (24)
Imechapishwa: 18/09/2026
https://firqatunnajia.com/ni-lazima-mtu-awe-ndani-ya-swalah-katika-duaa-ya-siku-ya-ijumaa/