Swali: Allaah amenineemesha neema kubwa ambayo ni kudhibiti swalah ya Fajr. Ninao ndugu wadogo ambao daima hufanya bidii waswali msikitini wote isipokuwa mmoja peke yake ambaye hajabaleghe. Wakati fulani hupitwa na Rak´ah moja ya swalah kwa sababu ya kuwatoa nje ya nyumba. Je, nina dhambi ikiwa sikuwaamrisha wakaswali?

Jibu: Ni lazima kwako kuwaamsha. Lakini unapaswa kuyatanguliza hayo mapema kidogo ili usipitwe na swalah. Tanguliza mapema kidogo kwa kiwango cha usipitwe na kitu katika swalah.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (17)
  • Imechapishwa: 16/10/2020