Ni lazima kuoga kwa aliyetokwa na manii kidogo sana?

Swali: Ikiwa mtu ataota ndoto ya kujamiiana na akatoka kiasi kidogo sana cha manii, tone moja au mawili, je, anaruhusiwa kuyaondoa kwa maji tu bila kuoga josho la janaba?

Jibu: Ikiwa mtu ataota ndoto ya kujamiiana na akaona maji, kwa maana ya manii, hata ikiwa ni tone moja tu, basi ni wajibu kwake kuoga josho.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/295)
  • Imechapishwa: 14/11/2026