Josho la janaba halisihi mpaka mtu akojoe kwanza?

Swali: Ndugu mmoja amenifahamisha kwamba muislamu anapomjamiiana mke wake basi ni lazima akojoe kabla ya kuoga josho. Vinginevyo ataendelea kuwa katika hali ya janaba, kwa sababu manii yaliyobaki kwenye dhakari hayaondolewi isipokuwa kwa mkojo, kama alivyonieleza ndugu huyo muislamu. Ni yepi maoni yenu kuhusu jambo hilo?

Jibu: Bali josho lake ni sahihi hata kama hakukojoa. Ikiwa atakojoa baada ya hapo, kisha kikamtoka kitu cha manii peke yake au pamoja na mkojo bila shahawa, basi si wajibu kwake kuoga josho mara ya pili. Inamtosheleza kufanya kujisafisha kwa maji na kutawadha kwa namna iliyowekwa katika Shari´ah.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/298-299)
  • Imechapishwa: 14/11/2026