Ni lazima kuamka na kuoga josho la janaba au naweza kuoga baadaye?

Swali: Ikiwa mtu atalala baada ya swalah ya Fajr na akaota ndoto ya kujamiiana, je, anatakiwa kuamka na kuoga josho wakati huo, ingawa bado ana muda wa kutosha wa kupumzika, kwa maana haujafika wakati wa swalah? Ninakusudia baada ya swalah ya Fajr, katika moja ya siku za mwezi mtukufu wa Ramadhaan.

Jibu: Si wajibu kwa aliyoota ndoto ya kujamiiana baada ya swalah ya Fajr kuoga josho kabla ya kuingia wakati wa swalah ya Dhuhr.

  • Muhusika: al-Lajnah ad-Daaimah
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa al-Lajnah ad-Daaimah (5/299-300)
  • Imechapishwa: 14/11/2026