Ni lazima kulipa deni la Ramadhaan kwa kufululiza au inafaa kwa kuachanisha?

Swali: Ni ipi hukumu kwa yule ambaye amekula Ramadhaan nzima na akataka kuilipa; je, ailipe kwa kufululiza au hakuna ubaya akailipa pindi anapotaka lakini hata hivyo kabla ya kuingia Ramadhaan ya kufuata?

Jibu: Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) amesema:

وَمَن كَانَ مَرِيضًا أَوْ عَلَىٰ سَفَرٍ فَعِدَّةٌ مِّنْ أَيَّامٍ أُخَرَ

“Atakayekuwa mgonjwa au safarini basi atimize idadi katika siku nyinginezo.”[1]

Allaah (Tabaarak wa Ta´ala) hakusema kwa kufululiza. Iwapo Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) angelitaka kufanya hivo kwa kufululiza basi angelifungamanisha. Kama alivosema (Ta´ala) kuhusu kafara ya kumfananisha mke na mgongo wa mama:

فَمَن لَّمْ يَجِدْ فَصِيَامُ شَهْرَيْنِ مُتَتَابِعَيْنِ

“Yule asiyepata, basi afunge miezi miwili mfululizo.”[2]

Mtu ambaye ana deni la Ramadhaan yuko huru; anaweza kulipa kwa mwezi siku mbili, siku tatu, siku nne au akazikusanya zote. Muhimu asiingiliwe na Ramadhaan ya pili isipokuwa baada ya kumaliza deni lake la Ramadhaan iliyopita. ´Aaishah amesema:

“Nilikuwa na deni la Ramadhaan na siwezi kulilipa isipokuwa katika Sha´baan.”

[1] 02:185

[2] 04:92

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: al-Liqaa’ ash-Shahriy (49) http://binothaimeen.net/content/1132
  • Imechapishwa: 02/06/2020