Swali: Vipi kuhusiana na kukubali zawadi?

Jibu: Ni jambo linahitaji kuangaliwa vyema. Kilichotangaa kwa wanazuoni ni kwamba inapendeza. Ni juu ya mpewaji kukubali zawadi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akikubali zawadi na akitoa malipo juu yake, kwa maana ya kwamba akitoa kitu badala yake. Kwa sababu baadhi ya watu wanaweza kutoa zawadi kwa kutaka badala. Kwa hivyo wakimpa zawadi na yeye anatoa badala yake. Hadiyth nyingine inasema:

“Peaneni zawadi mpendane.”

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/23863/هل-قبول-الهدية-واجب-ام-مستحب
  • Imechapishwa: 23/05/2024