Ni lazima kuinua mikono juu wakati wa kuomba du´aa?

Swali: Kuhusu du´aa ni lazima anyanyue mikono yake baina ya adhaana na Iqaamah au amwombe tu Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala)?

Jibu: Kuinua mikono ni miongoni mwa sababu za kukubaliwa du´aa. Lakini katika sehemu ambazo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) hakuinua mikono yake, haifai kuinua. Hakuwa (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiinua mikono yake baada ya kumaliza swalah za faradhi, katika Khutbah ya ijumaa wala Khutbah ya ´Iyd. Lakini katika kuomba mvua alikuwa akiinua mikono yake. Vivyo hivyo katika Khutbah ya ijumaa ikiwa anaomba mvua. Hali kadhalika katika du´aa nyinginezo. Ama katika swalah za faradhi hakuwahi (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiinua mikono baada ya kumaliza, baina ya sijda mbili wala mwishoni mwa Tashahhud.

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31199/هل-يلزم-رفع-اليدين-عند-الدعاء
  • Imechapishwa: 11/10/2025