Ni lazima Hajj aiambatane na tawbah ya kweli

Swali 35: Tumesema kuhusu Hajj kwamba inafuta madhambi na anarudi mwenye kuhiji kama siku aliyozaliwa na mama yake. Hadiyth ambayo ndani yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alimwambia Swahabah ambaye aliweka sharti kwamba asamehewe yaliyopita, akamwambia:

”Je, hukujua kwamba Uislamu unafuta yaliyokuwa kabla yake na kwamba Hajj inafuta yaliyokuwa kabla yake?”

Je, katika hili kuna dalili kwamba hata madhambi makubwa pia husamehewa kwa kufanya Hajj?

Jibu: Dhahiri ya Hadiyth:

“Yeyote atakayehiji na asifanye upuuzi wala kufanya ufuska… ”

Ikiwa atatimiza kigezo hiki.

”… basi atarudi kutoka kwenye madhambi yake kama siku aliyozaliwa na mama yake.”[1]

Vilevile Hadiyth ya ´Amr bin al-´Aasw (Radhiya Allaahu ´anh) ambayo umeiashiria:

”Hakika Hajj inafuta yaliyokuwa kabla yake.”

dhahiri yake ni ujumla na hivyo inafuta kila kitu isipokuwa kufuru. Kwa hiyo ni lazima ndani yake kuwe na tawbah.

[1] al-Bukhaariy (1521) na Muslim (1350).

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (21/39-40)
  • Imechapishwa: 25/05/2026