Ni ipi hukumu ya mtu kuswali peke yake nyuma ya safu?

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu kuswali peke yake nyuma ya safu?

Jibu: Kuna tofauti. Maoni ya sawa ni kwamba swalah haisihi. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Hana swalah yule mwenye kuswali peke yake nyuma ya safu.”

Shaykh-ul-Islaam na kundi la wanachuoni wengine wamesema:

“Haijuzu isipokuwa kwa dharurah.”

Maoni ni ya sawa ni kwamba swalah haisihi. Ni wajibu kwa mtu kutafuta nafasi katika safu ajiunge na maamuma, aswali kuliani kwa imamu au asubiri. Asipoweza yote hayo basi aswali peke yake na hapo swalah yake itasihi. Katika hali hiyo anakuwa ni mwenye kupewa udhuru. Haya ndio maoni ya sawa.

Watu wengi wanachukulia suala hili wepesi na wala hawamvuti yeyote. Kuhusiana na Hadiyth inayosema:

“Mvuteni mtu.”

ni dhaifu kwa mujibu wa wanachuoni. Maoni ya sawa ni kwamba swalah haisihi isipokuwa pale ambapo mtu mwingine atawahi kuswali pamoja naye kabla [imamu] hajasujudu. Hapo swalah itasihi. Vinginevyo airudi swalah yake.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (05) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191110#219240
  • Imechapishwa: 27/09/2018