Ni ipi hukumu ya mtu akichukia jambo la dini lakini halipingi?

Swali: Ni ipi hukumu ya mtu akichukia jambo lakini halipingi?

Jibu:

ذَٰلِكَ بِأَنَّهُمْ كَرِهُوا مَا أَنزَلَ اللَّـهُ فَأَحْبَطَ أَعْمَالَهُمْ

“Hivyo kwa sababu wao wameyachukia ambayo ameteremsha Allaah, basi akayaporomosha matendo yake.”[1]

Mwenye kuchukia kitu kilichoteremshwa na Allaah matendo yake yanaharibika. Mwenye kuchukia swalah japokuwa ataswali, akachukia hajj japokuwa atahiji, akachukia uharamu wa uzinzi au uharamu wa pombe matendo yake yote yanaporomoka.

Swali: Vipi akichukia ufugwaji wa ndevu?

Jibu: Hili ni jambo linahitaji kutazamwa vizuri. Ni jambo lina utata. Kwa sababu baadhi ya wanachuoni wanaona kuwa si lazima. Lakini mwenye kuchukia Shari´ah ya Allaah anakufuru. Kwa sababu angalau kwa uchache mtu anaweza kuwa ni Sunnah.

[1] 47:09

  • Mhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Kashf-is-Shubuhaat, uk. 105-106
  • Imechapishwa: 15/08/2019