Swali: Ni ipi hukumu ya kuvaa baadhi ya mavazi yaliyo na picha za viumbe wenye roho kama mfano wa mavazi ya mazoezi? Inafaa kucheza na mfano wa mavazi kama haya?

Jibu: Haifai kwa mtu kutumia mavazi yaliyo na picha. Ikiwa picha ina kichwa au ni picha kamilifu basi aharibu kile kichwa. Akiharibu kichwa basi hakuna neno. Akiswali katika nguo ilio na picha wapo katika wanachuoni waliosema kwamba swalah yake si sahihi. Wapo wanachuoni wengine waliosema kwamba swalah yake ni sahihi japokuwa anapata dhambi. Haya ndio maoni ya sawa. Lakini kwa hali yoyote mtu anapaswa ajiepushe na nguo zilizo na mapicha. Inahusiana na picha za viumbe vyenye roho; kama mfano wa picha za wanyama, mtu, ndege, wadudu au nyangumi. Hazijuzu isipokuwa pale atapoharibu na kukiondosha kichwa chake. Akiondosha kichwa chake basi hakuna neno.

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (04) http://audio.islamweb.net/audio/index.php?page=FullContent&audioid=191047#191047
  • Imechapishwa: 07/09/2018