Ni ipi hukumu ya kuoga kwa ajili ya ijumaa?

Swali: Ni ipi hukumu ya kuoga kwa ajili ya siku ya ijumaa?

Jibu: Kuoga kwa ajili ya siku ya ijumaa imependekezwa. Hadiyth inasema:

“Mwenye kutawadha siku ya ijumaa ni jambo zuri na mwenye kuoga [basi ifahamike kwamba] kuoga ndio bora.”

Kwa hivyo imependekezwa.

Swali: Kuoga kwa ajili ya siku ya ijumaa kunaanza baada ya swalah ya Fajr au baada ya kuchomoza kwa jua?

Jibu: Aoge pale anapotaka kwenda kuswali swalah ya ijumaa ili aondoshe jasho na harufu mbaya. Kwa vile ataenda katika mkusanyiko na msikitini, basi ni vizuri akajisafisha na akaondosha uchafu na jasho.

  • Mhusika: Imaam Swaalih bin Fawzaan al-Fawzaan
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Ighaathat-il-Lahfaan (88) https://www.alfawzan.af.org.sa/sites/default/files/igahssat.mp3
  • Imechapishwa: 08/09/2018