Swali: Ni ipi hukumu ya kukunuti katika swalah ya Fajr?
Jibu: Ni Bid´ah. Isipokuwa wakati wa majanga – katika hali hiyo kutaletwa Qunuut katika swalah zote. Hivo ndivo jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya, kama ilivyo katika Hadiyth ya Ibn ´Umar, Abu Hurayrah na wengineo.
Ama kufanya hivo kuwa ni maalum katika Fajr, Abu Maalik Sa´d bin Twaariq bin Ushaym al-Ashja´iy alimuuliza baba yake:
“Ee baba yangu kipenzi! Uliswali nyuma ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr na ´Umar. Je, walikuwa wakikunuti?” Akasema: “Ee mwanangu kipenzi, ni uzushi.”
Kuhusu Hadiyth ya Anas katika “as-Sunan” inayosema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliendelea kukunuti mpaka alipoaga dunia.”
ni dhaifu. Hadiyth hiyo imepitia kwa Abu Ja´far ambaye kuna maoni tofauti juu yake. Maoni yenye nguvu ni kwamba ni mnyonge.
Namshauri ndugu muulizaji arejee katika “Zaad-ul-Ma´aad” kwa sababu hakuna mfano wake katika maudhui haya. Hata watunzi wengine, akiwemo ash-Shawkaniy katika “Nay-ul-Awtwaar” na as-Swan´aaniy katika “Subul-us-Salaam” wanarejesha katika kitabu hichi chenye thamani ambacho ni “Zaad-ul-Ma´aad”.
- Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 322
- Imechapishwa: 29/04/2025
Swali: Ni ipi hukumu ya kukunuti katika swalah ya Fajr?
Jibu: Ni Bid´ah. Isipokuwa wakati wa majanga – katika hali hiyo kutaletwa Qunuut katika swalah zote. Hivo ndivo jinsi Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) alikuwa akifanya, kama ilivyo katika Hadiyth ya Ibn ´Umar, Abu Hurayrah na wengineo.
Ama kufanya hivo kuwa ni maalum katika Fajr, Abu Maalik Sa´d bin Twaariq bin Ushaym al-Ashja´iy alimuuliza baba yake:
“Ee baba yangu kipenzi! Uliswali nyuma ya Mtume wa Allaah (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam), Abu Bakr na ´Umar. Je, walikuwa wakikunuti?” Akasema: “Ee mwanangu kipenzi, ni uzushi.”
Kuhusu Hadiyth ya Anas katika “as-Sunan” inayosema:
“Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) aliendelea kukunuti mpaka alipoaga dunia.”
ni dhaifu. Hadiyth hiyo imepitia kwa Abu Ja´far ambaye kuna maoni tofauti juu yake. Maoni yenye nguvu ni kwamba ni mnyonge.
Namshauri ndugu muulizaji arejee katika “Zaad-ul-Ma´aad” kwa sababu hakuna mfano wake katika maudhui haya. Hata watunzi wengine, akiwemo ash-Shawkaniy katika “Nay-ul-Awtwaar” na as-Swan´aaniy katika “Subul-us-Salaam” wanarejesha katika kitabu hichi chenye thamani ambacho ni “Zaad-ul-Ma´aad”.
Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 322
Imechapishwa: 29/04/2025
https://firqatunnajia.com/ni-ipi-hukumu-ya-kukunuti-katika-swalah-ya-fajr/