Ni ipi hukumu ya kubakiza kucha zaidi ya siku arubaini?

Swali: Ni ipi hukumu ya kubakiza kucha zaidi ya siku arubaini?

Jibu: Hili linahitajia upambanuzi. Ikiwa yule mfugaji anataka kuwaiga makafiri waliopinda kutokamana na maumbile yaliyosalimika, basi kitendo hicho ni haramu. Kwa kuwa Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema:

“Mwenye kujifananisha na watu basi yeye ni katika wao.”

Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) amesema:

“Dogo liwezalo kusemwa kuhusu Hadiyth hii ni kwamba ni haramu japokuwa udhahiri wake unapelekea katika ukafiri wa yule mwenye kujifananisha.”

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (11/132)
  • Imechapishwa: 30/06/2017