Ni ipi hekima ya kuharamishwa nyama ya nguruwe?

Swali: Ni ipi hekima katika kuharamishwa nyama ya nguruwe?

Jibu: Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) amesema:

قُل لَّا أَجِدُ فِي مَا أُوحِيَ إِلَيَّ مُحَرَّمًا عَلَىٰ طَاعِمٍ يَطْعَمُهُ إِلَّا أَن يَكُونَ مَيْتَةً أَوْ دَمًا مَّسْفُوحًا أَوْ لَحْمَ خِنزِيرٍ فَإِنَّهُ رِجْسٌ

“Sema: “Sipati katika yale niliyofunuliwa Wahy kwangu kilichoharamishwa kwa mlaji kukila isipokuwa kiwe ni nyamafu [mzoga] au damu inayomwagika au nyama ya nguruwe – kwani hiyo ni uchafu.”[1]

Neno (الرجس) maana yake ni najisi na kitu kichafu. Hiyo ndiyo hekima katika kuharamishwa nyama ya nguruwe. Kwa sababu hiyo makafiri miongoni mwa manaswara na wengineo wameihalalisha kwa uchafu wao. Hekima ya Allaah (Subhaanahu wa Ta´ala) imekusudia kwamba vitu vichafu ni kwa ajili ya watu wachafu na wachafu wanawake ni kwa ajili ya wachafu wanaume.

[1] 6:145

  • Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (23/22)
  • Imechapishwa: 22/02/2026