Swali: Je, inafaa kwa mwanamke kutoka mbele ya wanawake wengine akiwa amevaa nguo fupi, nguo yenye kuonyesha kifua, nguo nyepesi au nguo yenye kubana?
Jibu: Sioni kuwa inafaa kwa mwanamke kutoka mbele ya wanawake wenziwe akiwa amevaa nguo fupi, nguo yenye kuonyesha kifua, nguo nyepesi au nguo yenye kubana. Kwa sababu yote hayo yanaweza kuwa yanaingia ndani ya maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
“Kuna watu aina mbili wa Motoni sijawaona: wanaume walio na bakora kama mkia wa ng´ombe ambazo wanawapiga kwazo watu, na wanawake waliovaa vibaya, uchi, waliopinda na wanawapindisha wengine. Vichwa vyao ni kama nundu ya ngamia. Hawatoingia Peponi na wala hawatonusa harufu yake. Harufu yake inapatikana umbali wa kadhaa na kadhaa.”[1]
Wanazuoni wamesema kuwa maana ya:
“Waliovaa vibaya, uchi.”
ni kwamba wanavaa nguo zenye kubana, nguo nyepesi au nguo fupi. Ilikuwa ni miongonim wa uongofu wa Mawahabah wa kike (Radhiya Allaahu ´anhunna) wanavaa nguo zinazofika kwenye nyayo za miguu na zinazofika viwiko vya mikono. Isipokuwa wanapoenda sokoni ndio huvaa nguo inayoshuka chini ya hapo na inayoshuka mpaka kwenye viganja vya mikono au wanavaa vifuniko vya mikono. Hakika miongoni mwa uongofu wa Maswahabah wa kike ni kuvaa vifuniko vya mikono. Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) amesema kuhusu mwanamke anapofanya Ihraam:
“Asivae vifuniko vya mikono.”
Ingelikuwa jambo la kuvaa vifuniko vya mikono halikuwa linatambulika katika wakati ule basi kusingelikuwa na haja ya kukataza katika hali ya Ihraam.
[1] Muslim (2128) na Ahmad (2/356).
- Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/280-281)
- Imechapishwa: 07/04/2026

Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/280-281)
Imechapishwa: 07/04/2026
https://firqatunnajia.com/nguo-fupi-nyepesi-au-yenye-kubana-kwa-mwanamke/