Swali: Je, inajuzu kwa mwanamke kuonyesha kitu katika kifua chake, mikono yake au miguu yake mbele ya wanawake?

Jibu: Hapana neno kuonyesha mikono yake mbele ya wanawake wengine. Vivyo hivyo kuhusu shingo na kichwa chake. Hata hivyo nawashauri wanawake jambo moja: Kila ambavo nguo ni yenye kupwaya na kumstiri zaidi, ndio kunamnufaisha zaidi. Tunawakataza kuigiliza yale yaliyoko katika magazeti haya ya sasa na hivyo wakayafuata. Kwa sababu mambo hayo yanampelekea mwanamke kujifananisha na wanawake wa kikafiri, ni mamoja analiridhia hilo au haliridhii. Kila ambavo mwanamke atakuwa ni mwenye kujisitiri ndio bora zaidi. Shaykh-ul-Islaam Ibn Taymiyyah (Rahimahu Allaah) ametaja namna ambavo wanawake wa kiswahabah walikuwa wakivaa kanzu zenye kuwafunika kuanzia kwenye viganja vya mikono mpaka kwenye nyayo za miguu, kuanzia viwiko vya mikono hadi miguuni. Hivi ndio bora.

  • Muhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Majmuu´-ul-Fataawaa (12/280)
  • Imechapishwa: 11/04/2026