Nenda kwa daktari wa kiume lakini uwe na Mahram

Swali: Mwanamke ana ugonjwa katika kizazi tangu miaka miwili. Ameenda kutibiwa kwa madaktari wanawake wema, lakini hakupata kupona. Kisha akamsikia daktari mwanaume. Je, inajuzu kwake kutibiwa kwake?

Jibu: Ikiwa hakupata mwingine isipokuwa yeye na yuko katika hali ya ulazima, hakuna ubaya. Anatakiwa awe pamoja naye Mahram kwa sababu ya udharurah. Ikiwa atapata mwanamke, basi asitibiwe kwa mwanaume.

  • Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
  • Imechapishwa: 07/10/2026