Swali: Ikiwa mtu anataka kusafiri na muadhini akatoa adhaana, je, analazimika kubaki na kuswali pamoja na mkusanyiko? Ikiwa atasafiri, je, anaweza kukusanya swalah hii pamoja na inayofuata na kuifupisha?
Jibu: Hili linahitaji maelezo. Ikiwa hana mtu wa kusafiri pamoja naye, basi anatakiwa kuswali. Ikiwa yuko pamoja na msafiri wenzake na anaogopa kwamba watamkosa, basi asafiri pamoja nao, kisha waswali nje ya mji. Wakiswali nje ya mji, watafupisha swalah. Aidha wanaweza kukusanya pamoja na swalah nyingine ikiwa ni miongoni mwa swalah zinazoweza kukusanywa pamoja, kama mfano wa Dhuhr pamoja na ´Aswr, Maghrib pamoja na ´Ishaa. Kinachozingatiwa ni mahali ambapo swalah inatekelezwa; ikiwa ataiswali akiwa mjini, ataswali kwa kukamilisha, na ikiwa ataiswali nje ya mji, basi ataiswali kwa kukusanya na kufupisha.
- Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
- Imechapishwa: 07/10/2026
Swali: Ikiwa mtu anataka kusafiri na muadhini akatoa adhaana, je, analazimika kubaki na kuswali pamoja na mkusanyiko? Ikiwa atasafiri, je, anaweza kukusanya swalah hii pamoja na inayofuata na kuifupisha?
Jibu: Hili linahitaji maelezo. Ikiwa hana mtu wa kusafiri pamoja naye, basi anatakiwa kuswali. Ikiwa yuko pamoja na msafiri wenzake na anaogopa kwamba watamkosa, basi asafiri pamoja nao, kisha waswali nje ya mji. Wakiswali nje ya mji, watafupisha swalah. Aidha wanaweza kukusanya pamoja na swalah nyingine ikiwa ni miongoni mwa swalah zinazoweza kukusanywa pamoja, kama mfano wa Dhuhr pamoja na ´Aswr, Maghrib pamoja na ´Ishaa. Kinachozingatiwa ni mahali ambapo swalah inatekelezwa; ikiwa ataiswali akiwa mjini, ataswali kwa kukamilisha, na ikiwa ataiswali nje ya mji, basi ataiswali kwa kukusanya na kufupisha.
Muhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: Fataawaa Mutanawwi´ah (26)
Imechapishwa: 07/10/2026
https://firqatunnajia.com/msafiri-kukusanya-na-kufupisha-inategemea-na-mahali-swalah-inatekelezwa/