Ndugu yake amechukua mkopo benki katika nyumba wanayoshirikiana

Swali: Ndugu wawili walishirikiana katika kujenga nyumba ambapo mmoja wao akachukua mkopo kutoka benki ilihali huyo ndugu mwingine alikuja kujua baada ya kumalizika jengo. Ni kipi kinachomlazimu huyo ndugu mwingine? Je, anapata dhambi?

Jibu: Nataraji kuwa hapati dhambi, kwa sababu hakujua. Dhambi zinampata yule mfanyaji. Aliyepewa mtihani kwa jambo hilo na si yeye mfanyaji, dhambi zinapata yule mtendaji.

  • Muhusika: ´Allaamah Muqbil bin Haadiy al-Waadi´iy
  • Tarjama: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Qam´-ul-Mu´aanid, uk. 289
  • Imechapishwa: 02/08/2025