Ndio maana vitabu vya historia ya Maswahabah vina vituko

Miongoni mwa madhehebu ya Ahl-us-Sunnah wal-Jamaa´ah ni kunyamazia yaliyopitika kati ya Maswahabah. Tusiyazungumze. Tupuuze, kwa mioyo yetu na ndimi zetu, yaliyopitika kati yao. Badala yake tuseme kuwa wote ni wenye kujitahidi. Aliyepatia katika wao anapata ujira mara mbili na aliyekosea katika wao anapata ujira mmoja. Huo ni Ummah ambao umeshatangulia. Wana waliyochuma na nyinyi mna mliyochuma. Hamtoulizwa kuhusu waliyokuwa wakitenda.

Lau mtu atasoma [vitabu vya] historia ataona vituko vikubwa! Ataona kuna ambao wako upande wa Banuu Umayyah na kumponda ´Aliy bin Abiy Twaalib na watu wa familia ya Mtume (´alayhis-Salaam). Ataona wengine wamevuka mipaka kwa ´Aliy bin Abiy Twaalib  na watu wa familia ya Mtume (´alayhis-Salaam) na anawaponda Banuu Umayyah. Hili ni kwa sababu katika historia kunaingia pia siasa.

  • Mhusika: Imaam Muhammad bin Swaalih bin ´Uthaymiyn
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: Sharh Riyaadh-is-Swaalihiyn (02/280-281)
  • Imechapishwa: 27/09/2024