Swali: Nini unawanasihi vijana ambao wameharibiwa na muda wa ziada na ukosefu wa kazi, simaanishi upotofu, bali kukaa majumbani kwa kula, kunywa na kukaa tu, jambo ambalo limesababisha udhaifu wa msukumo wa dini na ugumu wa nyoyo zao na kuchanganyikiwa?
Jibu: Tunawanasihi wamche Allaah, watafute elimu na waelekee katika Qur-aan kwa kujifunza, kutafakari na kuelewa. Aidha waelekee katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kujifunza katika shule na misikiti. Vielvile wakutane na ndugu wema na kushirikiana na watu wema ili wakumbushane Qur-aan Tukufu na Sunnah iliyotakasika.
Wawe na kazi ambazo wanawanufaisha watu. Ikiwa hawana ajira wajitahidi kupata kazi, viwanda wanavyovifanya au makampuni wanavyoanzisha wanajinufaisha wao na kuwanufaisha watu pamoja na kushikamana na kumcha Allaah na kuwa na juhudi katika kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama kubaki nyumbani kwa kulala, uvivu na udhaifu, hilo halimfai muumini. Inampasa awe na hima, awe na bidii na atafute kazi ambayo ataitumia kuwanufaisha watu na kujinufaisha yeye mwenyewe, kama kilimo, viwanda vinavyowanufaisha watu, kuanzisha makampuni yanayowanufaisha watu ili kuwe na manufaa kwa watu na kwake yeye na kujaza muda huu wa ziada na kuondoa upotevu wa muda unaomdhuru na haumfaidii.
Swali: Je, akiamrisha mema barabarani na katika vikao, je, hilo linaweza kuondoa muda wa ziada?
Jibu: Hilo ni katika kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa ana elimu na ana wivu wa dini, kutembea katika njia na kuamrisha mema na kukataza mabaya na kulingania watu, hii ni kazi kubwa, ni kazi njema na inaondoa sehemu kubwa ya muda wa ziada.
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3334/نصيحة-للشباب-حول-الفراغ-والبطالة
- Imechapishwa: 30/09/2026
Swali: Nini unawanasihi vijana ambao wameharibiwa na muda wa ziada na ukosefu wa kazi, simaanishi upotofu, bali kukaa majumbani kwa kula, kunywa na kukaa tu, jambo ambalo limesababisha udhaifu wa msukumo wa dini na ugumu wa nyoyo zao na kuchanganyikiwa?
Jibu: Tunawanasihi wamche Allaah, watafute elimu na waelekee katika Qur-aan kwa kujifunza, kutafakari na kuelewa. Aidha waelekee katika Sunnah za Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) na kujifunza katika shule na misikiti. Vielvile wakutane na ndugu wema na kushirikiana na watu wema ili wakumbushane Qur-aan Tukufu na Sunnah iliyotakasika.
Wawe na kazi ambazo wanawanufaisha watu. Ikiwa hawana ajira wajitahidi kupata kazi, viwanda wanavyovifanya au makampuni wanavyoanzisha wanajinufaisha wao na kuwanufaisha watu pamoja na kushikamana na kumcha Allaah na kuwa na juhudi katika kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ama kubaki nyumbani kwa kulala, uvivu na udhaifu, hilo halimfai muumini. Inampasa awe na hima, awe na bidii na atafute kazi ambayo ataitumia kuwanufaisha watu na kujinufaisha yeye mwenyewe, kama kilimo, viwanda vinavyowanufaisha watu, kuanzisha makampuni yanayowanufaisha watu ili kuwe na manufaa kwa watu na kwake yeye na kujaza muda huu wa ziada na kuondoa upotevu wa muda unaomdhuru na haumfaidii.
Swali: Je, akiamrisha mema barabarani na katika vikao, je, hilo linaweza kuondoa muda wa ziada?
Jibu: Hilo ni katika kumtii Allaah na Mtume Wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam). Ikiwa ana elimu na ana wivu wa dini, kutembea katika njia na kuamrisha mema na kukataza mabaya na kulingania watu, hii ni kazi kubwa, ni kazi njema na inaondoa sehemu kubwa ya muda wa ziada.
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3334/نصيحة-للشباب-حول-الفراغ-والبطالة
Imechapishwa: 30/09/2026
https://firqatunnajia.com/nasaha-kwa-vijana-wenye-kuzurura-na-wasio-na-kazi/