Swali: Ni ipi hukumu ya ujambazi? Je, mtu akitubu kabla ya kukamatwa katika ujambazi, je, adhabu itatekelezwa juu yake?
Jibu: Ujambazi ni katika maovu makubwa. Ni kule kuwavamia watu njiani na kutoka dhidi ya watu kwa silaha ili kuchukua mali zao. Hili linaitwa ujambazi na wenye kiueneza maharibifu ardhini. Nao hutoka dhidi ya watu kwa silaha kwa aina mbalimbali za silaha, hata kwa marungu katika miji, njiani au jangwani ambapo wanawakabili watu kwa silaha au marungu au hata kwa mikono yao kwa mujibu wa maoni sahihi. Hata kama hawana silaha, kwa nguvu tu ambapo wanachukua mali za watu kwa nguvu. Hawa huitwa majambazi. Mtawala anapaswa kuwashughulikia kwa yale aliyoyataja Allaah katika Kitabu Chake:
إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ أَوْ يُنفَوْا مِنَ الْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا عَلَيْهِمْ ۖ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
”Hakika si vyenginevyo malipo ya wale wanaompiga vita Allaah na Mtume Wake na wakapania kufanya ufisadi katika ardhi, wauawe au wasulubiwe au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha au watolewe katika nchi. Hayo ndio malipo yao duniani na Aakhirah watapata adhabu kuu; isipokuwa wale waliotubia kabla ya kuwatia mbaroni. Basi tambueni ya kwamba hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]
Hao ndio majambazi. Mtawala anapaswa kuwafuatilia kwa nguvu, kujitahidi kuwatafuta na kuwakamata na kuwahukumu kwa yale Allaah aliyoyaweka katika Shari´ah ili wasiharibu katika ardhi na ili wasiharibu usalama.
[1] 05:34
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3329/ما-هو-حد-الحرابة-وما-حكم-من-تاب-قبل-ان-يقدر-عليه
- Imechapishwa: 30/09/2026
Swali: Ni ipi hukumu ya ujambazi? Je, mtu akitubu kabla ya kukamatwa katika ujambazi, je, adhabu itatekelezwa juu yake?
Jibu: Ujambazi ni katika maovu makubwa. Ni kule kuwavamia watu njiani na kutoka dhidi ya watu kwa silaha ili kuchukua mali zao. Hili linaitwa ujambazi na wenye kiueneza maharibifu ardhini. Nao hutoka dhidi ya watu kwa silaha kwa aina mbalimbali za silaha, hata kwa marungu katika miji, njiani au jangwani ambapo wanawakabili watu kwa silaha au marungu au hata kwa mikono yao kwa mujibu wa maoni sahihi. Hata kama hawana silaha, kwa nguvu tu ambapo wanachukua mali za watu kwa nguvu. Hawa huitwa majambazi. Mtawala anapaswa kuwashughulikia kwa yale aliyoyataja Allaah katika Kitabu Chake:
إِنَّمَا جَزَاءُ الَّذِينَ يُحَارِبُونَ اللَّـهَ وَرَسُولَهُ وَيَسْعَوْنَ فِي الْأَرْضِ فَسَادًا أَن يُقَتَّلُوا أَوْ يُصَلَّبُوا أَوْ تُقَطَّعَ أَيْدِيهِمْ وَأَرْجُلُهُم مِّنْ خِلَافٍ أَوْ يُنفَوْا مِنَ الْأَرْضِ ۚ ذَٰلِكَ لَهُمْ خِزْيٌ فِي الدُّنْيَا ۖ وَلَهُمْ فِي الْآخِرَةِ عَذَابٌ عَظِيمٌ إِلَّا الَّذِينَ تَابُوا مِن قَبْلِ أَن تَقْدِرُوا عَلَيْهِمْ ۖ فَاعْلَمُوا أَنَّ اللَّـهَ غَفُورٌ رَّحِيمٌ
”Hakika si vyenginevyo malipo ya wale wanaompiga vita Allaah na Mtume Wake na wakapania kufanya ufisadi katika ardhi, wauawe au wasulubiwe au ikatwe mikono yao na miguu yao kwa kutofautisha au watolewe katika nchi. Hayo ndio malipo yao duniani na Aakhirah watapata adhabu kuu; isipokuwa wale waliotubia kabla ya kuwatia mbaroni. Basi tambueni ya kwamba hakika Allaah ni Mwingi wa kusamehe, Mwenye kurehemu.”[1]
Hao ndio majambazi. Mtawala anapaswa kuwafuatilia kwa nguvu, kujitahidi kuwatafuta na kuwakamata na kuwahukumu kwa yale Allaah aliyoyaweka katika Shari´ah ili wasiharibu katika ardhi na ili wasiharibu usalama.
[1] 05:34
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/3329/ما-هو-حد-الحرابة-وما-حكم-من-تاب-قبل-ان-يقدر-عليه
Imechapishwa: 30/09/2026
https://firqatunnajia.com/hukumu-ya-majambazi/