Swali: Nini unachomshauri mtu aliyepatwa na wasiwasi mwingi katika wudhuu´ na ndani ya swalah?
Jibu: Tunamshauri ajikinge kwa Allaah dhidi ya shaytwaan. Aseme:
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ مَلِكِ النَّاسِ إِلَـٰهِ النَّاسِ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ´
”Sema: ”Najilinda na Mola wa watu, mfalme wa watu, mwabudiwa wa haki wa watu, kutokamana na shari za anayetia wasiwasi, mwenye kurejea nyuma, anayetia wasiwasi nyoyoni mwa watu miongoni mwa majini na watu.”[1]
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ
“Pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan, basi mtake kinga Allaah.”[2]
Kuna Maswahabah walimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ee Mtume wa Allaah! Hakika shaytwaan ananichanganya swalah yangu.” Huyo alikuwa ni ´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha:
”Jikinge kwa Allaah dhidi ya shaytwaan mara tatu na tema cheche za mate upande wako wa kushoto mara tatu.”
´Uthmaan akasema: ”Nikafanya hivyo, basi Allaah akaondoa nilichokuwa nikihisi.”
Swali: Ni kitabu gani bora kilichoandikwa kuhusu jambo hili?
Jibu: Sikumbuki chochote kwa sasa, lakini kitabu cha Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ”Ighaathat-ul-Lahfaan min Wasaawisi ash-Shaytwaan” ni kizuri.
Swali: Ateme cheche za mate ndani ya swalah yenyewe?
Jibu: Ndio, ndani ya swalah yenyewe.
Swali: Ageuke upande wake ndani ya swalah na ateme?
Jibu: Ndio, ndani ya swalah yenyewe. Upande wake wa kushoto kidogo.
[1] 114:01-06
[2] 07:200
- Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
- Tarjama: Firqatunnajia.com
- Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31576/ما-النصيحة-للمبتلي-بالوساوس-في-الوضوء-والصلاة
- Imechapishwa: 09/11/2025
Swali: Nini unachomshauri mtu aliyepatwa na wasiwasi mwingi katika wudhuu´ na ndani ya swalah?
Jibu: Tunamshauri ajikinge kwa Allaah dhidi ya shaytwaan. Aseme:
قُلْ أَعُوذُ بِرَبِّ النَّاسِ مَلِكِ النَّاسِ إِلَـٰهِ النَّاسِ مِن شَرِّ الْوَسْوَاسِ الْخَنَّاسِ الَّذِي يُوَسْوِسُ فِي صُدُورِ النَّاسِ مِنَ الْجِنَّةِ وَالنَّاسِ´
”Sema: ”Najilinda na Mola wa watu, mfalme wa watu, mwabudiwa wa haki wa watu, kutokamana na shari za anayetia wasiwasi, mwenye kurejea nyuma, anayetia wasiwasi nyoyoni mwa watu miongoni mwa majini na watu.”[1]
وَإِمَّا يَنزَغَنَّكَ مِنَ الشَّيْطَانِ نَزْغٌ فَاسْتَعِذْ بِاللَّـهِ
“Pindi utakapokuchochea uchochezi kutokana na shaytwaan, basi mtake kinga Allaah.”[2]
Kuna Maswahabah walimwambia Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam):
”Ee Mtume wa Allaah! Hakika shaytwaan ananichanganya swalah yangu.” Huyo alikuwa ni ´Uthmaan bin Abiyl-´Aasw. Ndipo Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akamwamrisha:
”Jikinge kwa Allaah dhidi ya shaytwaan mara tatu na tema cheche za mate upande wako wa kushoto mara tatu.”
´Uthmaan akasema: ”Nikafanya hivyo, basi Allaah akaondoa nilichokuwa nikihisi.”
Swali: Ni kitabu gani bora kilichoandikwa kuhusu jambo hili?
Jibu: Sikumbuki chochote kwa sasa, lakini kitabu cha Ibn-ul-Qayyim (Rahimahu Allaah) ”Ighaathat-ul-Lahfaan min Wasaawisi ash-Shaytwaan” ni kizuri.
Swali: Ateme cheche za mate ndani ya swalah yenyewe?
Jibu: Ndio, ndani ya swalah yenyewe.
Swali: Ageuke upande wake ndani ya swalah na ateme?
Jibu: Ndio, ndani ya swalah yenyewe. Upande wake wa kushoto kidogo.
[1] 114:01-06
[2] 07:200
Muhusika: Imaam ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah bin Baaz
Tarjama: Firqatunnajia.com
Marejeo: https://binbaz.org.sa/fatwas/31576/ما-النصيحة-للمبتلي-بالوساوس-في-الوضوء-والصلاة
Imechapishwa: 09/11/2025
https://firqatunnajia.com/nasaha-kwa-mwenye-wasiwasi-wakati-wa-kutawadha-na-wakati-wa-kuswali/