Nasaha kwa mfungaji juu ya kuchunga mambo ya wajibu kukiwemo swalah

Miongoni mwa mambo yaliyokokotezwa kwa mfungaji ahifadhi mambo ya faradhi na ya wajibu. Baadhi ya watu wanapofunga wanatumia vibaya mambo ya wajibu. Ukifunga ni lazima utekeleze mambo ya wajibu na mambo ya faradhi. Miongoni mwa faradhi ambazo ni muhimu sana ni swalah ambayo Allaah ameifaradhisha juu ya waja Wake. Hii ndio faradhi na wajibu mkubwa baada ya Tawhiyd. Hakika jambo la swalah ni kubwa. Allaah (´Azza wa Jall) alimfaradhishia nayo Mtume wake (Swalla Allaahu ´alayhi wa sallam) akiwa juu ya mbingu ya saba. Mara ya kwanza kulifaradhishwa swalah khamsini kisha zikapunguzwa mpaka swalah tano. Ni lazima kuziswali swalah kwa wakati wake.

Baadhi ya watu wanapofunga wanalala wakati wa Dhuhr, ´Aswr na wanaamka wakati jua linapozama. Kadhalika swalah ya Fajr wanakula katikati ya usiku kisha wanalala na kuamka baada ya jua kuchomoza. Huyu ina maana kwamba amefunga kwa hawaa na matamanio yake. Huyu si mja wa Allaah. Mja wa Allaah ni yule anayetekeleza faradhi kwa wakati wake. Unatakiwa kujipanga viziru ili uweze kutekeleza faradhi za Allaah. Usiwe mja wa hawaa na matamanio yako. Ni lazima uswali Fajr katika mkusanyiko. Huna ruhusa ya kuswali baada ya jua kuchomoza. Ni mamoja katika Ramadhaan na miezi mingine. Kadhalika Dhuhr na ´Aswr pia watakiwa kuziswali ndani ya wakati wake. Haifai kwako ukazikusanya Dhuhr na ´Aswr na ukaziswali karibu na wakati wa jua kutaka kuzama. Huku ni kujifananisha na wanafiki.

Wapo wanachuoni wenye kuona kwamba mtu akichelewesha swalah mpaka ukatoka wakati wake pasi na udhuru basi haikubaliwi. Kundi la wanachuoni wengine wameona kwamba anakuwa kafiri. Muheshimiwa Shaykh ´Abdul-´Aziyz bin Baaz (Rahimahu Allaah) anaona kwamba yule ambaye siku zote anaswali Fajr baada ya jua kuchomoza na haweki bidii yoyote… kama mfano wa ambaye anaweka alamu ya kuamka wakati wa kwenda kazini kwamba swalah yake anarudishiwa mwenyewe na kwamba anakufuru. Anaona kuwa swalah yake haisihi hata kama baadaye ataiswali mara elfumoja. Hii sio ile swalah aliyoamrishwa. Jengine hana udhuru; si kwamba amesahau, ni mwenye kupindisha maneno, mwenye kupewa udhuru wala kwamba amepitikiwa na usingizi na hivyo anapewa udhuru. Bali amefanya hivo kwa kukusudia. Kwa ajili hii wapo wanachuoni wenye kuona kwamba mwenye kuchelewesha kipindi cha swalah kimoja tu kwa makusudi amekufuru. Dalili wametumia ni maneno yake Mtume (Swalla Allaahu ´alayhi  wa sallam):

”Mwenye kuacha swalah ya ´Aswr matendo yake yameharibika.”

Hakuna mtu ambaye matendo yake yanaharibika isipokuwa kafiri tu. Amesema (Ta´ala):

وَمَن يَكْفُرْ بِالْإِيمَانِ فَقَدْ حَبِطَ عَمَلُهُ وَهُوَ فِي الْآخِرَةِ مِنَ الْخَاسِرِينَ

”Yeyote atakayekanusha imani, basi hakika yameharibika matendo yake naye Aakhirah atakuwa miongoni mwa waliokhasirika.”[1]

[1] 5:5

  • Mhusika: ´Allaamah ´Abdul-´Aziyz bin ´Abdillaah ar-Raajihiy
  • Mfasiri: Firqatunnajia.com
  • Marejeo: http://shrajhi.com.sa/uploads/rmadhan_02.mp3
  • Imechapishwa: 07/05/2019